Kususa haijawahi kuwa suluhu... Vyama vingine vinashiriki.
Lissu ana roho mbaya sana, kwa kuwa yeye hana cheo chochote, anafanya juu chini na wenzake wakose, hata kesi ya akina mdee ni yeye ndio anashinikiza ili wakose ubunge, kwenye bunge la Afrika mashariki pia amezuia ili wakose wote
Na kwanini mshiriki wakati mnajua mnasindikiza kabisa
Msusie msisusie, mfoke msifoke, mlie msilie, mnune msinue, mbweke msibweke, haiwasaidii kitu maana kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Wabunge watapatikana tuu hata wote wakitoka CCM. Nyinyi mtabaki kufoka tu wenzenu wanacheka na nyavu! Kama baadhi ya vyama vimeshakubali kushiriki, CHADOMO ni mdudu gani mbele ya umma wa kitanzania! Leo watasema hawashiriki, kesho utashangaa wanakinga bakuli la njaa ya ruzuku! Hawa ni njaa tupu sasa hivi, hawana mbele wala nyuma wala kushoto wala kulia!
Wanajua ngoma iliyo mbele yao maana wanaelewa kuwa wanaenda kuwa wasindikizaji hawa CHADOMO, wakithubutu kutia mguu hawapati hata kura ya kujipigia wenyewe, watakuta wanampigia mtu mwingine!
Mbunge Aida Kenani yupo bungeni kwa uchaguzi ule wa 2020. Logically haipo sawa kutoa sababu ya uchaguzi wa 2020 kama kigezo cha kususia uchaguzi wa wabunge wa EALA
Afterall, wabunge wa CCM kamwe hawatamchagua mgombea kutoka CHADEMA. So, uamuzi wa kususia ni mzuri tu maana uwaokolea fedha na muda ambao wangeupoteza kufanya kampeni. Na hii ndio sababu halisi ya kususia
Mbunge Aida Kenani yupo bungeni kwa uchaguzi ule wa 2020. Logically haipo sawa kutoa sababu ya uchaguzi wa 2020 kama kigezo cha kususia uchaguzi wa wabunge wa EALA
Afterall, wabunge wa CCM kamwe hawatamchagua mgombea kutoka CHADEMA. So, uamuzi wa kususia ni mzuri tu maana uwaokolea fedha na muda ambao wangeupoteza kufanya kampeni. Na hii ndio sababu halisi ya kususia
Ukisusa wenzako,wanakula.
Hivi maana ya kususa ni ipi hasa.Mnyika ametoa sababu.Sasa huko kususa kunaingiaje kwenye hoja hizo?Using'ang'anize mambo.Hawajateua wagombea kwa sababu zao.Basi.
Mtu anayekwenda kinyume na maamuzi ya chama huwa anapuuzwa? Ni mtizamo wako though.
Hayo unayasema wewe!
Nyie endeleeni kususa mpaka mtakapojitambua itakuwa mmezeeka pia!
Nimechanganyikiwa.
Wamesusa kwa Sababu hawatambui nini?
Kwa mantiki hiyo hawata ingia kwenye vinyanganyiro vya Uchaguzi 2025??
Sielewi.
Sidhani kama ulisoma nilichoandika?Sababu zao zipi?. Mbona mnawalazimisha kuteua. Nakumbuka uchaguzi wa 2020 mliwafungia ofisi na kuwaengua wagombea ubunge wa Chadema zaidi ya hamsini. Leo mnajifanya kuwalazimsha wateue Kama mlivyowalaghai akina Mdee. Endeleeni na CCM ya too achaneni na chadema.
CHADEMA panahitajika Viongozi hawa tulio nao hawajielewiKatibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho hakitashiriki uchaguzi wa kuwapata wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashiriki (Eala).
Uchaguzi huo utafanyika katika mkutano wa Bunge la Tanzania utakaoanza Septemba 13, 2022 jijini Dodoma.
Mnyika amesema vikao vya Chadema bado havijajadili msimamo wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambao walisema matokeo yake hawayatambui.
Katibu Mkuu huyo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 5, 2022 wakati akizungumza na Mwananchi Digital, kuhusu ushiriki wa wao Eala baada ya vyama vya ACT - Wazalendo na CUF kukamilisha mchakato wa uteuzi wa majina ya wagombea wao watakaowakilisha vyama hivyo katika uchaguzi huo.
Wakati ACT-Wazalendo na CUF vikiteua wagombea wao leo Jumatatu CCM inamalizia mchakato wa uhakiki wa majina ya wagombea wao waliowasilisha vielelezo na sifa za kuwania ubunge wa Eala.
“Hatutashiriki, vikao vya chama havijabadili bado msimamo wetu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tunasisitiza kuharakishwa kwa mchakato wa kupata KatibaMpya, Tume Huru ya Uchaguzi.
“Pia kushughulikia wa athari na madhara yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa 2020. Ni vema dhamira ya kufungua ukurasa mpya kuonyeshwa kwa haraka kwa masuala yenye kuhitaji utekelezaji wa Katiba na sheria mfano haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara,” amesema Mnyika.
Mbali na hilo, Septemba 14, mwaka 2021 Chadema kilisusia uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, kikisisitiza hakitashiriki mchakato wowote hadi Tume Huru ya uchaguzi itakapopatikana.
Pia Chadema kilisusia kikao cha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa na wadau wa demokrasia uliofanyika jijini Dodoma na kufunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Makonda au Sabaya??CHADEMA panahitajika Viongozi hawa tulio nao hawajielewi