Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Jeshi la Polisi leo tarehe 22 Novemba, 2024 katika Pori la Halungu lililopo Wilaya ya Mbozi wamevamia Msafara na kumkamata Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Viongozi mbalimbali aliokuwa ameambatana nao.
Msafara wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ulikuwa umeshafanya Mikutano ya kampeni katika Kata ya Itaka, Kijiji Cha Itewe na Kata ya Halungu Mjini.
Awali mkutano wa kwanza uliokuwa ufanyike katika mji wa Mlowo uliozuiliwa na Polisi pamoja na wenyeji wetu ambao ni Chama Cha ACT Wazalendo kutualika kushiriki kwenye mkutano wa pamoja ila Polisi walikataa na kutawanya wananchi Kwa mabomu ya machozi.
Kabla ya kuwakamata walifuatwa na gari ya Polisi ambayo ilikutana nao njiani na hivyo iligeuza na baada ya mwendo kidogo walikuwa njia imefungwa na gari za polisi ndipo walipofungua milango Kwa nguvu na kuanza kuwashambulia waliokuwa kwenye Magari hayo na kuwakamata Kwa nguvu.Waliokamatwa ni:
1. Mhe.Freeman Mbowe
2. Mhe. Joseph Mbilinyi - Mwenyekiti Kanda ya Nyassa
3. Mhe. Pascal Haongo- Mbunge wa Mbozi mashariki Mstaafu
4. Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Wilaya ya Mbozi
5. B Appolinary Boniface - Mkuu wa Digital platform
6. Paul Joseph - Afisa habari Kanda ya Nyassa6. Calvin Ndabila - Afisa habari Kanda ya Nyassa
7. Mdude Nyagali - Mwanaharakati na mwanachama wetu
8. Wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa Bwire, Adamoo na Lingwenya
Jeshi la Polisi wameondoka na viongozi wetu na hajajasema wanawapeleka wapi na mpaka Sasa hatujui wanashikiliwa wapi na Kwa sababu gani.
Soma Pia: