GE2025 CHADEMA yatoa tamko kuhusu sakata la Timu ya Yanga kuchangia Harambee ya CCM

GE2025 CHADEMA yatoa tamko kuhusu sakata la Timu ya Yanga kuchangia Harambee ya CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nimejiridhisha akili za viongozi wa Yanga ni damaged beyond repair. Ile kauli ya Manara itaishi milele
Hakika upo sahihi, imagine kiongoz wa taasisi anatudanganya kumleta manzoki kumbe ilikua bosheni kwaajil ya uchaguz? Imagine kiongoz wa taasisi sekta ya habari anatujaza mashabiki na wanachama eti linakuja chezaji refu kuliko goli? Linakuja chezaji bahari itasogea mpaka Moro? Anakuja mchezaj bahari itakauka? Linakuja chezaji umeme utakatika nchi nzima? Kweli?
 
Nimejiridhisha akili za viongozi wa Yanga ni damaged beyond repair. Ile kauli ya Manara itaishi milele
Wewe ndiyo damaged beyond repair. Angalia bendera ya CCM. Angalia bendera ya Yanga. Angalia bendera ya Mufti. Uhuru wa Nchi hii uliletwa na TANU, Yanga, na Waislamu wa tangia Kariakoo na Magometi Kota na Mtoni kwa Aziz Ali, hii hadi Mlandizi. Hii ni historia huwezi kuikwepa. Kama huwezi kuikwepa huwezi kuivunja. Hata kwa mabeberu mabwana zao CHADEMA, West Ham United ni ya Lord May wa Conservative, Celtic ni ya Kanisa Katoliki, na Newcastle United ni ya coalminers wa Labour Party. FIFA wanajua hilo hawawezi kufanya kitu, kwa sasa Yanga ni kama bado iko vitani na mabeberu ukoloni mambokeo kupitia FIFA. Kama huipendi Yanga toka.
 
Usikute huyu ni kiongozi wa Yanga au CCM..umethibitisha kauli yangu kwamba ni damaged beyond repair. Ni wa kuchoma moto tu
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Klabu ya Yanga kujiepusha na Siasa na kurejesha Shilingi milioni 100 zinazodaiwa kuchangia kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia GSM Foundation.

Kupitia taarifa iliyotolewa Agosti 15, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, CHADEMA imesema kitendo cha Yanga kuhusishwa na mchango huo ni kuingiza michezo kwenye siasa, jambo linalokiuka kanuni za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zinazokataza vilabu kujihusisha na siasa

CHADEMA imesema michezo inapaswa kuunganisha watu wa itikadi na mitazamo tofauti, na si kuwa chombo cha kugawa wananchi. Chama hicho kimeongeza kuwa hatua ya Yanga kusaidia chama kimoja cha siasa ni kuwadhalilisha mashabiki na wanachama wasio na itikadi sawa

Aidha, chama hicho kimewataka viongozi wa Yanga kujitathmini iwapo wana uhalali wa kuongoza taasisi inayokusudiwa kuunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kisiasa.

CHADEMA WANA ROHO MBAYA ZA KWANINI YAANI WAMEONA CCM WANAFAIDI SANA YAANI MPAKA AIBU KWAKUWA WAO HAWAJAWAHI KUCHANGIWA NA YANGA AIBU KWAOOO
 
Kama mnashindwa tu kutofautisha kati ya GSM na Young Africans Sports Club bado mnajiita akili kubwa? FIFA sio wajinga. Wanajua TFF kuna usajili wa Young Africans Sports Club na sio GSM. Pigeni kelele lakini hakuna FIFA itafanya kwa Yanga.
Umepuuzwa. Hunaga akili
 
Ninamshauri Brenda awe ana-proofread kabla ya ku-share. Taarifa ina makosa mengi ya uandishi.
Afadhali wewe una akili huru umeliona hilo. Kuna mpigwa tone tone mmoja hapo juu #12 eti amesifia kuwa barua imeenda shule kimoja 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom