CHADEMA yatuma salamu za rambirambi kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha maafa huko Hanang

CHADEMA yatuma salamu za rambirambi kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha maafa huko Hanang

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa chama cha kwanza cha siasa Nchini Tanzania kutuma rambirambi zilizoambatana na salamu za pole kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea huko Hanang na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20 , huku watu wengine wakiwa hawajulikani walipo.

Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 49

Taarifa yao hii hapa.

View attachment 2832366
Hii itakuwa imeandikwa na Mbowe mwenyewe kwa sababu imeandikwa kwa busara sana. Siku nyingine mumpe Lema au Mdude awaandikie.
 
Sasa wale wauza sura wanaotumia magari ya umma wamesaidia nini zaidi ya kupiga picha na tope ?
Sasa hiyo si ni opportunity kwenu kufanya kitu cha maana kwa wananchi badala ya kukalia mchakato ?!
Kuna tofauti gani kati yenu na wauza sura kama na nyie hamfanyi kitu, badala yake mmekalia mchakato?
Ok, leo ni siku ya 3 baada ya mafuriko kutokea, mchakato umefikia harua gani?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa chama cha kwanza cha siasa Nchini Tanzania kutuma rambirambi zilizoambatana na salamu za pole kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea huko Hanang na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20 , huku watu wengine wakiwa hawajulikani walipo.

Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 49

Taarifa yao hii hapa.

View attachment 2832366
Naunga mkono Salaam hizi, niliwahi kushauri
Japo kazi ya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga kila kitu. Kwenye maslahi ya taifa, tutangulize utaifa, tuwe wamoja, wakweli na tusipotoshe, hivyo this is a good start, kwenye majanga ya Kitaifa, we stand as one!.
Big up sana Chadema for this!.
P
 
Usilete siasa kwenye masuala ya maafa na maisha ya watu. Ndio shida yenu ninyi Machadema kuleta siasa hadi kwenye vifo vya watu utafikiri mnaombeaga nakusubili maafa na majanga yatokee ili mpate hoja ,hasa baada ya kuwa na ukame wa hoja na kufirisika kisera kwa chama Chenu.

Nani kakwambia kuna mashindano ya kutoa salamu za pole na rambirambi mpaka useme mmekuwa wa kwanza?

Kwani sasa hujuwi kinachoendelea na kinachopiganiwa ni kuokoa maisha ya watu,kutafuta waliopotea na hawajulikani walipo,kutoa huduma za haraka kwa majeruhi,kuzuia na kuwaondoa walio katika maeneo hatarishi zaidi,kutoa misaada ya kibinadamu kwa ambao makazi yao yameharibiwa na kusombwa na maji?

Kazi hiyo imeanza kufanywa na CCM mkoa tangia zilipotoka taarifa ya janga hilo.hiyi ndio kazi inayoendelea kufanywa na CCM kwa kushirikiana na wananchi wa huko,tofauti na ninyi mnaipiga porojo huku mkiwa kwenye makochi yenu na kunywa mipombe yenu.

Acheni na msilete siasa kwenye maisha ya watanzania,ndio maana mnapuuzwa sana na watanzania.nani kawaambieni kuna riadha ya kuwahi kutoa taarifa za pole.kwa sasa riadha iliyopo ni kuokoa maisha ya watu na kuwasaidia wahanga.

Ndio maana Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan yupo njiani kurejea nchini ili aende eneo la tukio na wakati huo huo tayari ameshatoa maagizo mazito yaliyowatetemesha watendaji wa serikali ili wafike haraka sana eneo la tukio.
Kile kile uchosema hasilete yaani siasa na wewe ndicho ulicholeta yaani siasa kwenye maisha ya watu hanang

Na wewe wahi katesh kapige selfie kama hao viongozi wako wa chama ili tujue na wewe ulikuwepo.
 
😆😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom