Uchaguzi 2020 CHADEMA yawasha moto Mbeya Mjini, mjumbe wa kamati Kuu aanza ziara ya kutoa semina kata zote, hii hapa ni kata ya Nzovwe

Uchaguzi 2020 CHADEMA yawasha moto Mbeya Mjini, mjumbe wa kamati Kuu aanza ziara ya kutoa semina kata zote, hii hapa ni kata ya Nzovwe

CHADEMA NI MPANGO WA MUNGU HADI NABII SHILLA AMELITHIBITISHA HILO[emoji3577][emoji3577]SWALA.
Kwenye biblia na Quran hkuna mtu anaitwa nabii Shilla labda Ni nabii wa chama saccos
 
Sijawahi waamini watanzania kwenye kile kibox cha kupiga kura...ni wanafiki sana!
 
Mbozi, Tanzania

Fikra Huru Za Watanzania

Uimara wa CHADEMA na imani yao wananchi kwa chama ni thabiti sana. Ndugu unaitwa ujiunge na CHADEMA ili Maendeleo ya Watu na Demokrasia ya nchi, mkoa, wilaya, tarafa, kata , mtaa, familia na mtu mmoja mmoja yatimie.
 
Julai 2020
Tunduma, Tanzania

MWAKAJOKA Atikisa Tunduma
"Mkutano wa kuwashukuru Wananchi "CHADEMA Tutashinda Uchaguzi Majimbo Yote 2020 .



Mfano Chipaka tenki la maji na matenki mengine yatasambaza huduma ya maji safi kwa wote.

Elimu mji wa Tunduma imezidi kuboreshwa

Mbunge wenu mimi Mwakajoka nimetambuliwa ktk hansard ya bunge kama mchangiaji bora aliyeshika namba 7 ktk bunge la Muungano wa Tanzania kuwatetea wakulima, wafugaji, wavuvi na watumishi wa umma siyo Tunduma tu bali pia kuwatetea waTanzania wote. Kiasi Spika Job Ndugai akawa anaomba nipunguze mbinyo kuibana serikali lakini mimi kama Mwakajika nilikuwa sielewi wala kuchoka kulibana bunge la Ndugai na serikali ya CCM Mpya.

Michezo ni afya na ajira mfano Mwakajoka Cup imesaidia kutoa burudani na kutoa vijana 3 waliochaguliwa kwenda under 17 timu ya taifa ya Tanzania ya soka.

Mfuko wa jimbo 95 milioni kila kata imenufaika kufuatana na mahitaji ya kila sehemu.

Vituo vya Afya pia vimeboreshwa kutoa huduma kwa Mama na Mtoto pia vijana na kina baba.
Source : JAY TV
 
Sugu aka moto chini amekwisha hana mvuto tena, sijui wana Mbeya walimchaguaje mvuta bangi mkubwa huyu anaejitaja yeye mwenyewe katika wimbo hapo chini !! sasa tunaona wazi Sugu has the last kick of a dying horse!! msela wetu Sugu kalidhalilisha sana bunge badala ya kutunga sheria alipayuka na kuropoka tu kwa miaka mitano sikuwahi kumsikia akitaja elimu, maji wala barabara za Mbeya mjini nitamkumbuka zaidi kwa burudani aliyoitoa bungeni akiimba wimbo ANA MIAKA KUMI NA NANE!!



 
5 Julai 2020
Tunduma, Tanzania

Humphrey Polepole apigishwa gwaride

Katibu Uenezi wa CCM Mpya Taifa Humphrey Polepole ilibidi aigize miondoko ya Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu jukwaani kwa mtindo wa 'kufokafoka' na gwaride la Lucky Dube wa South Afrika na wana Tuunduma ili angalau aambulie kupata wanachama 'wapya' 350


Source : Jay TV
 
Julai 2020
Tunduma, Tanzania

Mkutano wa ndani wa CHADEMA
Mjini wa Tunduma wasitisha shughuli kumpokea Mh. Frank Mwakajoka aliporejea jimboni toka Dodoma kuwawakilisha wananchi kwa kuikumbusha serikali majukumu yake kwa wananchi na moja kwa moja kwenda kufanya mkutano wa ndani na wananchi.


Frank Mwakajoka awashitaki kwa wananchi Mawaziri 3 wa serikali ya CCM Mpya waliotumwa kumrubuni ahamie CCM kuunga juhudi ili awe mbunge wa CCM Mpya lakini awahakikishia kuwa alikataa rushwa hiyo.

Anaendelea , Pia niliandikiwa ki memo nionane na kiongozi wa shughuli za Bunge wa CCM pia nilikataa katakata kuonana naye.
source : DSS Tunduma
 
3 Julai 2020
Tunduma, Tanzania

Frank Mwakajoka - Hakuna kulala shughuli lazima ziendelee.

Nilipokuwa bungeni niliipiga kibano serikali lazima ijenge hospitali kubwa Tunduma na huduma ya maji safi ktk mji huu muhimu lango la kwenda kusini mwa Afrika na kuiunganisha na bandari ya Dar es Salaam


Source : DSS Tunduma
 
Julai 2020
Mbeya Tanzania

WanaMbeya wamhakikishia Sugu wapo pamoja naye 2020

Waimba na kufurahia kumuona Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU mwakilishi wao, mtetezi wa haki ya Maendeleo na Demokrasia kwa wote kupitia CHADEMA. Wamtia moyo Sugu na kumpa pole kwa kufanya kazi ktk mazingira ya sasa gandamizi lakini wamhimiza aendelee kuwatumikia waTanzania kwani Sugu ni kipenzi cha wote.

 
Back
Top Bottom