Hata kama ni 1%, hii ina maana 1% wakilipia, system itakuwa na uwezo wa ku absorb 1% more ya wale wasioweza kujilipia, au (kwa mfano kama tukitimiza ndoto ya kusomesha wote, asiwepo asiyejiweza ambaye atakosa nafasi) hata kupeleka hizo funds katika kusomesha wasiojiweza vyuo vikuu, au hata kutumia hizo funds katika social services nyingine. Tusitake kujifanya kama tushamaliza matatizo yetu yote na hii elimu mpaka form six ndilo tatizo letu la mwisho, si kweli, tunahitaji kila senti tutakayoweza kuipata, serikali yetu haina fedha kwa hivyo. Na hata tukiweza kuongeza mapato ya kodi kuna mambo lukuki yanaisubiri kodi hiyo hiyo. Barabara, umeme, maji, afya you name it. Sasa kwa nini tusiwalipishe watu wenye uwezo wa kulipa?
Ni rahisi sana ku dismiss kwamba wenye uwezo ni wachache, lakini je ushawahi kujiuliza ungejisikiaje kama wewe ndiye ungekuwa huna uwezo halafu mwenye uwezo kachukua nafasi yako ?
Leo tukisema tuue Mtanzania hata mmoja utasema mtu mmoja ni idadi ndogo sana ukilinganisha na watanzania ? Vipi kama tukiamua kwamba mtu mmoja huyu awe wewe?
Kitu cha kujadili hapa, ni kwamba mwenye uwezo kujilipia kutolipishwa ni sawa au si sawa, one only has to look at our private schools and the type of lifestyles some kids live, hivi tunataka kujitwika mizigo ya kusomesha wote hawa bila sababu ya msingi ?