Chaguzi mbili kuu pale unapogundua mkeo anakusaliti

Ndio maana nimeweka hayo machaguzi mawili, kuachana naye ama kumsamehe ni maamuzi tu ya mhanga.
 
Mkuu, option ni moja tu, Achana nae, hiyo ya pili utakaribisha maradhi nyumbani once a cheater always a cheater
Mkuu soma vizuri kuhusu hiyo option ya pili utaona wazi kilichomo, hakikushawishi wewe uliyesamehe uendelee kushiriki tendo la ndoa na huyo mzinzi.

Unamsamehe, ni ex kwako Ila ni mama ya watoto wako unaweza kumkaribisha home kusalimia watoto, huo ndio msamaha wenyewe, hampaswi kuwa maadui baada ya kumsamehe.
 
Mkuu, achana na hizo mambo, mwanamke anaye cheat ni hatari kuliko AK 47. KAA NAYE MBALI
 
Be careful what you wish for
 
Umeongea ukweli,kama mtu anauhusiano wa kingono nje ya ndoa maandiko yanaruhusu kutoa talaka ukitaka,lakini pia ukiamua kumsamehe ni wewe tu. Mathayo19:9" Ninawambia kuwa mtu yeyote anayemtaliki mke wake isipokuwa kwasababu ya uasherati,na kumwoa mwingine,anafanya uzinzi".
 
Hapo weweumechagua njia moja tu ya msamaha hujaweka ama kuijadili option ya pili ya divorce.
 
Usidanganye watu,Yesu hakuamuru kuwasamehe wanawake waasherati,kazi ya kumsamehe mwanamke muasherati ni ya Mungu pekee.Mwanaume kumsamehe mwanamke muasherati na mzinzi ni kuingilia majukumu ya Mungu
 
Mwanaume kumsamehe mwanamke muasherati na mzinzi ni kuingilia majukumu ya Mungu
Maneno kama haya..... "Utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyo wasamehe waliotukosea... " Yanaelezea uhalisia wa kusamehe, ni Yesu mwenyewe aliyeelekeza tufanye hivyo.

Wewe unapopinga kusamehe , maana yake ni kwamba humkubali Yesu.
 
Hapo weweumechagua njia moja tu ya msamaha hujaweka ama kuijadili option ya pili ya divorce.
Talaka ipo kwenye options zote mbili...

1. Achana naye = mpe talaka...

2. MSAMEHE = unaweza kuzungumza naye japo(umemtaliki) umeachana naye, hiyo ndiyo maana yake.
 
Sitisha mahusiano tu,Kila mmoja aendelee na mishe zake za siri lakini msiachane mlee vijana!

Niliiona Kwa mwamba mmoja hivi!

Hiyo ni njia bora zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…