Chaguzi mbili kuu pale unapogundua mkeo anakusaliti

Chaguzi mbili kuu pale unapogundua mkeo anakusaliti

1. ACHANA NAYE na ulee watoto wako uliowapata ukiwa na mkeo. Unaweza kuamua kuoa mwanamke mwingine ama kubaki mseja daima.

Kumbuka ukiamua kuoa tena hutapata malaika mwingine bali utapata mke mwenye moyo kama wa yule utakayemuacha.

2. MSAMEHE mkeo kisha tafuta mtaalam wa kukusaidia kushughulika kuponya maumivu yako.

Weka mkakati wa namna bora ya kukusaidia usiingie katika mahusiano mapya.

Leeni watoto wenu pamoja hata kama mu wanandoa mliochana.

Vile utakavyo amua ni chaguo, huyo mwanamke ni mkeo ulimpenda ukamuoa, ni chaguo lako.

Kwa upande wangu binafsi ningechagua njia ya MSAMAHA kwa sababu mimi ni zao la msamaha. Yesu mwenyewe alisisitiza MSAMAHA 7×70 na wala hakusisitiza talaka, hivyo mie ninaishi ndani ya msamaha.

Pamoja na kumsamehe lakini ikitokea akaendeleza - maisha ya uzinzi - udanganyifu wa kudumu - hapo nitamwangusha kama kizazi cha moto. Lakini sitavunja ndoa yangu kwa sababu ya wingu linalopita.

Tafadhali usiue wala usijiue kwa sababu ya mkeo kukucheat bali chagua hatua mojawapo kati ya hizo mbili nilizozitaja.

Ubarikiwe.
Barikiwa mkuu,you have said it all
 
Nilichokuja kugundua kwanini wanaume wengi sana wanateseka na mapenzi au mahusiano , wanaume wanachukulia mahusiano ya uchumba au ndoa serious sana kuliko wanawake ifike muda tubadilike kuepusha matatizo yanayoweza kutokea pale upendo wa mwanamke unapoisha
 
Usidanganye watu,Yesu hakuamuru kuwasamehe wanawake waasherati,kazi ya kumsamehe mwanamke muasherati ni ya Mungu pekee.Mwanaume kumsamehe mwanamke muasherati na mzinzi ni kuingilia majukumu ya Mungu
Si kweli!
Kwamba kazi ya kusamehe ni ya mungu kwenye swala la uzinzi! Ni lako mhusika kabisa,mungu anaheshimu sana privacy za watu, na maamuzi ya mtu ! Ndo maana katupa uhuru kumkiri yeye kama mungu au kifo cha milele, hapa hamlazimishi yoyote,huyu ndo mungu anaitwa mungu wa haki,na upendo.. lakini swala la mzinzi kama ataomba msamaha kwa mungu atasamehewa hata kama wew hujasamehe na ukamuacha


Ni kweli

Kwamba mungu karuhusu talaka ,kwa habari ya uzinzi tu si vinginevyo! Lakini kama utasema nimemsamehe mungu anaheshimu hilo,lakini pia ukisema hujamsamehe na ukalala nae, na ukaja muacha,! Basi huko uendako na kulala na mwanamke mwingine utakuwa unazini
 
Si kweli!
Kwamba kazi ya kusamehe ni ya mungu kwenye swala la uzinzi!
Umefafanua vizuri kabisa Ila hukuzingatia kanuni za uandishi na ukaandika mungu badala ya Mungu.

Jaribu ku edit uandike Mungu ili kuweka maana halisi ya ufafanuzi wako.
 
Back
Top Bottom