Chakula cha Rais

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Poleni na pilikapilika za Corona. Hongereni mliochangamkia fursa kwa kuuza vitakasha mikono.

Familia nyingi hasa hizi za kitajiri za madaraja ya A B na C wana utaratibu wa kutoa oda ya chakula cha kula kila siku mfano anaweza kutaka kupikwe ugali dagaa na mawese. Na wengine wanatabia ya kuingia mpaka jikoni.

Je, Rais naye anauwezo wa kuomba apikiwe ugali na mlenda na ntole ama vinapikwa vyakula vingi vya kila aina ya chakula cha kiafrika na pia kinachobaki kinaenda wapi au nae anakula viporo hasa uporo wa wali nazi na haragwe? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji39][emoji1787][emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa akili zako unafikiri kuwa rais ni mtu mwenye maisha mazuri sana! Kwa taarifa yako hakuna binadamu anaepata taabu hapa duniani kama raisi!
 
Akili za Jumapili baada ya kuamka na hang over.
 
Kwanini unawaza ulevi tu. Jumapili nimeamka na njaa ndio nikawaza mwenzetu anakula nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha kumbe njaa ndio inakufanya uwaze hivyo? Sorry kwa kukufikiria vinginevyo mkuu.
Basi jua kuwa anahisi njaa kama wewe na mimi tuhisivyo, anakula kama wewe na mimi tulavyo ila mkewe ndio anaamua leo ale nini na kesho ale nini. Utofauti ni kwamba chakula chake kinakaguliwa/kupimwa kabla hajala Ila mimi na wewe kikiwekwa mezani tu tunafakamia.
 
Anakulaga na wengine, kinapikwa zaidi ya kimoja, kikiletwa wasaidizi wake wanaonja( kuepuka sumu) maana watu si wema. Wakati anakula kilichobaki wanakula wengine. Sometimes anaweza kula na familiya yake kama sisi tunavyokula na wengine.
 
Kwa akili zako unafikiri kuwa rais ni mtu mwenye maisha mazuri sana! Kwa taarifa yako hakuna binadamu anaepata taabu hapa duniani kama raisi!
Sio kweli.
Embu tulia chini kwanza kabla hujaandika.
Hii sio akili yako bro tunakumanya
 
Ikulu Ni taasisi wale wapishi si wakumpikia yeye tuu. Tena wamerudi wengi tuu zaidi ya mwanzo kutokana na mahitaji kuongezea
 
sasa kikiwekwa sumu ya kukuua muda mrefu labda miezi sita, watagunduaje
Anakulaga na wengine, kinapikwa zaidi ya kimoja, kikiletwa wasaidizi wake wanaonja( kuepuka sumu) maana watu si wema. Wakati anakula kilichobaki wanakula wengine. Sometimes anaweza kula na familiya yake kama sisi tunavyokula na wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah...Mimi mwenyewe hapa ni Rais....Sasa sijui unamuongelea yupi? wa TFF, wa TBA...wa manzese au wa MGD???[emoji2960][emoji56]

Sent using Beretta ARX 160
 
Unachokiandika ndio mfumo wako wa akili unaonyesha jinsi utapiamlo ulivyoshambulia ubongo wako. Jifunze kwa wengine upate kuelimika sio kijidai wajua na mwerevu. Jifunze wa walimwengu na walimwengu wajifunze kwako. Soon naweza kufa kwa uzee na mafuriko ya huku kwetu bali pokea usia wangu.
Dah...Mimi mwenyewe hapa ni Rais....Sasa sijui unamuongelea yupi? wa TFF, wa TBA...wa manzese au wa MGD???[emoji2960][emoji56]

Sent using Beretta ARX 160

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…