Chakula gani ukipika watu wengine wanaomba kuongeza chakula tena?

...ohooo,....nishaandaa maji na mchele hapa, maji kidogo ndio kiasi gani?...na kikombe kimoja cha mchele.
Leo mpaka namimi nichemshe pilau yangu hapa!...
 
lol yaani wewe nyumbani kwako siwezi kufikia hata iweje, maana toka unanipokea terminal akili yangu itakuwa inawaza hii sredi lol...
Ila tunacompliketisha tu, hizi ni taaluma za watu naweka zangu professional beki 3 aliyesomea mapishi basi unakuwa na menu yako tu jikoni....
Tukaajili kaLizzy, au we unasemaje?
 
Mi na Kongs tunakuwazia yaliyomema, wala usiwaze bibie!

Hapo somo nimelielewa utamu hasa, ntalirudia taratibu nkirudi home na lile ricekuka niliweka kabatini 4 gud.
 
...ohooo,....nishaandaa maji na mchele hapa, maji kidogo ndio kiasi gani?...na kikombe kimoja cha mchele.
Leo mpaka namimi nichemshe pilau yangu hapa!...
Hahaha. . .
Haya fanya hivi. . .
Kwanza loweka mchele wako, alafu ndio ubandike maji jikoni. Chemsha vikombe viwili (size ile ile ulotumia kupima mchele) alafu yakishachemka punguza kimoja kabla ya kuweka mchele wako, usisahau mafuta na chumvi.

Acha moto wa juu kwa dakika kama tano hivi alafu angalia umelainika kiasi gani. Kama bado ni mgumu sana ongeza maji robo kikombe,punguza moto mpaka karibu na mwisho. . .kama jiko lina namba 1-6 weka namba 2 alafu funika. Ukishafunika hapo wala usiwe na haraka, unaweza ukaacha hata nusu saa, unaiva taratibu na hamna hofu ya kuunguza.
 
huo ndo ukweli
huwezi kuwa kamili kila idara kuna vitu vinasumbua

ila sio kwamba niko mweupe kabisa
nikikupikia samaki wa kukaanga, bilingaya pembeni na ugali utaimba haleluya

au kande la maharage
au mtori
au kideri au loshoroo
utanikubali tu

Mi na Kongs tunakuwazia yaliyomema, wala usiwaze bibie!

Hapo somo nimelielewa utamu hasa, ntalirudia taratibu nkirudi home na lile ricekuka niliweka kabatini 4 gud.

Hahahaha mna lenu jambo. . .eti nije kuwapikia. .MRINGE?

Jaribu bana. . .wali wa rice cooker haunogi kama wa kupika mwenyewe kwenye sufuria na ukipata mkaa upalie kabisa.
 
Hehehe! Umejuaje na weye kupika hujui!? Nawangoja wapishi mie, unikome!
Note: akija ashadii hapa patachimbukia!
osha, weka funga kwenye karatasi kama gazeti afu tia kwenye mfuko wa plastick

angalizo gazeti lina wino tafuta karatasi plain.
Cabbage sijajaribu mbinu hii
 
tena apalie mkaa hadi upate matandu

ungekuwa mmama, hayo matatu wayatia mchuzi anapewa mme ili alegee na kutoa siri au hela
hii ni pwani zaidi

nilikotoka ukimpa mme matandu na talaka juu
Hahahaha mna lenu jambo. . .eti nije kuwapikia. .MRINGE?

Jaribu bana. . .wali wa rice cooker haunogi kama wa kupika mwenyewe kwenye sufuria na ukipata mkaa upalie kabisa.
 
tena apalie mkaa hadi upate matandu

ungekuwa mmama, hayo matatu wayatia mchuzi anapewa mme ili alegee na kutoa siri au hela
hii ni pwani zaidi

nilikotoka ukimpa mme matandu na talaka juu

Sie huo ulikua kwaajili yetu watoto wakati tunasubiria muda wa kula ufike. Na wali ukishapakuliwa sufuria inanyunyuziwa mchuzi kidogo basi ule ukoko unavyonoga, mpaka raha.

Sie kwetu anachoweza kupewa baba kabla ya muda wa kula ni supu kidogo. . .chakula nusu nusu mwiko.
 
Hahaha! Wewe chizi fresh unajua!

Umenikumbusha nikiwa kibinti, nafundishwa kupika ugali. Mama anadai eti ukiiva ukipiga kitonge kiduchu ukutani kinaanguka. Basi kikinasa ukutani ujue haujaiva. Nilikuwa hadi nimalize kusonga ugali ukuta umeshaisha karibia nahamia mlangoni, lol!
tena apalie mkaa hadi upate matandu

ungekuwa mmama, hayo matatu wayatia mchuzi anapewa mme ili alegee na kutoa siri au hela
hii ni pwani zaidi

nilikotoka ukimpa mme matandu na talaka juu
 
yaani hakuna kitu kinanishinda dunia hii kama kupika,naweza tu uji
 
Wapishi bora na wazuri duniani ni wanaume ,wanawake ni wahudumu wazuri ila mapishi hawajui.
 
Yaani mi niende kumtembelea mtu (esp rafiki zangu) halafu aweke menu isiyoeleweka.......michuzi bahari.......walah namwambia. Ila ugenini ndio inakuwa ngumu kidogo............nitakula kidogo na kuaga saa hiyo nikatafute msosi kwingine nisishinde na njaa bure.
 
Uko vizuri Lizzy....mwanamke asiwe mvivu kukaangiza.....ndio sifa kubwa, sio yule anaekuagiza ukitoka mzigoni nichukulie chips kuku
 
Uko vizuri Lizzy....mwanamke asiwe mvivu kukaangiza.....ndio sifa kubwa, sio yule anaekuagiza ukitoka mzigoni nichukulie chips kuku
Hahahaah. . . eti 'ukitoka mzigoni nichukulie chips kuku!!'.Sindio maisha ya kimjini mjini hayo?
 
lizzy uko vizuri mama kumbe sector zote dah!
mm ktk ulivyotaja hapo juu najua baadhi hayo mapizza hata mm walaaa.
 
Wa kuoka sijawahi kula.

We LAT wewe. . . aisee mi crabs sijapata uthubutu wa kuonja kwakweli. Ladha yake ikoje?

Lizzy

yaani na mimi nilikuwa kama wewe, siku moja i got convinced, crab haina tofauti na samaki ya kawaida kabisaa, ndani ya zile legs na bones ndipo utakuta minofu, its rally delicious, ila minofu yake ipo in form of fibers

kama upo dar nenda chinese restaurant inaitwa TANGREN karibu na nyumba private ya kikwete hapo moroco, utafurahi, pia kuna maandazi ya mihogo, wachina bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…