Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Njugu mawe asee nilikula siku moja tuu nikiwa chaliii, aliyepika alikosea sijui.
 
Rosholoo (sijui nimepatia wachaga mnisaidie[emoji1][emoji1])
 
Choroko=Hii ilinikuta maeneo flani na hakukuwa option ya mboga nyingine ile kujaribu tu nikaamua kukaa na njaa.

Juisi ya Miwa=Ilikuwa Cafeteria chuoni, Ladha niliyoipata ni tofauti na matarajio na nilihisi Muuza juice kanifanyia makusudii, but wat for?!...juisi ya miwa ni mbaya tu.

Senene= Nilona kinyaa kula baada ya kushawishiwa sana nikala, ni watamu sana ila baadae nikajilaumu nimekula vipi panzi wale, sitarudii aki, Mwanza hiyo.

Ugali wa mhogo/udaga et al=Kwa bibi hiyo, Nilikula tonge moja tu mpango wa wali ulifanyika kumridhisha mjukuu.
 
Sesame rice. Kila nikienda mgahawa wa Wachina nahakikisha siagizi hiki.
 
Back
Top Bottom