Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Ukifika Nyasa kuna samaki anaitwa MBOFU, aisee huyo samaki sidhani kama nitamla tena
Anaitwa Mbufu!! Huyu raha yake umle kama mchemsho achanganywe na ndizi!! Hukuwakuta wataalamu wanaomjulia vyema kumpika
 
Mimi binafsi nilishakula vitu vingi sana na hakuna kilishawahi nikataa asee ..nakula Kila kilicho mbele na Sina historia ya tumbo kuvuruga Wala kuuma ..nakula chochote Kile kilichopikwa na binadamu na mazingira safi .
 
Dur
Kuna matunda Zanzibar kubwakubwa hivi kwa nje kama lina miiba lina harufu mbaya kama utumbo uliooza,nilitapika kisa ile harufu.......sijui jina ila lina bei kubwa.
Duriani/Doriani hahaaa . Kuna watu wa aina mbili moja wakilipenda watalila milele na wengine wakilichukia wanalichukia milele.

Hili ukilila unatakiwa ukae mbali na watu maana wanaweza hisi kuna mzoga
 
Mambo vipi wanaJF natumai mko poa. Kwenye misosi kuna kuwa na kile chakula una hamu nacho au tu umekuta sehemu kimepikwa kwasababu hujawahi kula unaamua kula huo msosi kwa mara ya kwanza lakini chakula hicho kina kushinda kabisa hata kukupelekea kujisikia vibaya.

Mimi miaka ya nyuma nilikuwa nasikiaga kuhusu supu ya kongoro siku na mimi nikaamua nijue ikovipi hiyo supu nikaenda sehemu nzuri tu nikaulizia nikaambiwa ipo basi nikaletewa pale nikaanza kuipiga lakini kidogo tu nilikula kama vipande viwili tu vya ile nyama nikajisikia kuchefuchefu vibaya sana hata hiyo nyama kumeza haimezeki nikaacha supu karibia yote pale hadi leo hii sitaki tena kusikia kuhusu hiyo supu

Nyingine hii ilikuwa ni juisi ile ya rozela nilikuta imetengenezwa sehemu nikanywa glasi moja ilikuwa na ladha nzuri tu lakini baada ya hapo nilijisikia vibaya sana kama kizunguzungu mara kama mwili unataka ku vibrate mara jasho linatoka japo kulikuwa na feni yaani ilikuwa ni shida mpaka leo nikiiona hiyo juisi naipitia mbali kabisa. Hata juisi ya miwa ilinishinda kabisa ni bora nile muwa kama muwa

Vipi kwa upande wenu wadau ni kitu gani ulikula lakini baada ya hapo hutaki tena kukila.
Ming'oko[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
3.KONGORO

natamanigi sana nikiona mtu anakula kongoro anahangaika na bomba lile,huku akpga kijiko cha supu,nahisi anakula kitu kitamu sana,siku moja isiyo na jina namimi nikaitsha kongoro,wapendwa hamna siku hela yangu iliniuma kiasi kwamba nikatamani kulia kama ile siku,maana ki ukweli lile kongoro ile nimeweka mdomoni tu nilirudsha chenchi,ikabd nisingizie naumwa,nikatoka eneo lile nikabadlisha kiwanja nikarudi kwenye supu zetu za ng'ombe.
Mkuu me unakosa vitu adimu sana asee
 
Back
Top Bottom