Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,092
Reaction score
53,496
Napenda sana kula vyakula jamii ya ngano kama;

1. Chapati

2. Maandazi

3. Half cakes

4.Tambi

5.Napenda mboga kama maharage, samaki sato, mchuzi mzito wa kuku

6.Napenda nyama ya kuku

7.Samaki au kitimoto

8.Nyama za aina nyingine si mpenzi nazo sana

9. Napenda sana juice ya mananasi au maembe

10.Napenda matunda kama ndizi, parachichi au papai.

Vyakula nisivyovipenda;

1.Makande

2.Dagaa

3.Maziwa mtindi

4.Mihogo ya kuchemsha

5.Dona

6.Mikate

7.Bamia

8.Matango

9.Pilipili ya aina yeyote

10.Nyanya chungu
 
Napenda pilau, wali maharage, ndizi nyama za kichagga, ugali na mboga za majani zilizochanganywa na nyama, wali samaki, wali nyama/kuku, makande ya nazi siku moja moja, ugali na dagaa zenye bamia na nyanya chungu,

kwa breakfast mkate na mayai ya kukaanga (spanish), sausage, vitumbua, maandazi na chai ya tangawizi, ndizi mzuzu na chapati maji/pan cake. Juice napendelea mixed fruits kama embe, passion, nanasi.
 
mie ugali tu na mboga yoyote yaani napenda sana.
ila mayai na vitu vinavyoandaliwa kutokana na mayai vimenikalia kushoto.pamoja na huyu samaki kibua nae kanishinda.
 
Napenda ndizi nyama, ndizi kuku, ndizi samaki, wali wa nazi kwa maharage na changu au nguru wa vipande alonona, biriani haswa ya nyama au kuku. Pilau si sana

vya ngano napenda bokoboko haswa la kuku, mikate ya maji, ikifuatiwa na buns then mikate ya ufuta.

Mayai, catles, eggchops,mtabak,msanif na mapochopocho yote yanopikwa kwa masamaki, manyama na mayai.

Napenda vyakula vingi vya sukari hasa vinopikwa kwa maziwa kama pudding, faluda, custard,cheese cake, boga, mumunye, tambi, kaimati, chila, vitumbua nk.

Nisije kusahau na ma pizza na ma burger, na ma hot dogs plus sandwich.

Yaani mi Bulldog na napenda kula vizuri na navijua vyakula.

Usije ukaniletea makande lkn wala dona, siyawezi.

Byeee.
 
Last edited by a moderator:

Good for you madame
 
Last edited by a moderator:
Napenda li ugali likubwa na samaki sato wa kuchoma,

Ugali dagaa roast

Wali maini

ndizi utumbo
SIPENDELEI
kabichi,

Maharage
Rumye mimi wali na ugali sipendi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom