Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Kusema ukweli siku nikila chakula hiki hio siku hua nzuri sana na ninaipenda japo hutokea mara chache!!asubuhi nile chai ya rangi au maziwa yenye harufu ya mchai chai, kitafunwa kiwe vitumbua vya ukweli,, mchana ugali mzuri wa sembe na dagaa za kigoma na mlenda wa bamia na majani ya maboga,, usiku nile wali maharage mchicha na kachumberi ya pilipili mbuzi! Na ndizi mbivu,, hio siku hua sina stress na sitaki mtu anipikie nipike mwenyewe!!
 
Mhhhhhh! Ni aje weye? Ugali kwa samaki wa kukaanga pembeni kuna mchicha wa nazi pilipili kichaa au mbuzi na gudulia la maji...Acha kabisa utaona mlima wa ugali unashuka tu ukimaliza unapiga glass sita zako za maji unajisikia raha mpaka kisogoni lol!

Umenisababishia njaa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mhhhhhh! Ni aje weye? Ugali kwa samaki wa kukaanga pembeni kuna mchicha wa nazi pilipili kichaa au mbuzi na gudulia la maji...Acha kabisa utaona mlima wa ugali unashuka tu ukimaliza unapiga glass sita zako za maji unajisikia raha mpaka kisogoni lol!
Bubu atasema
 
Haya lunch yako leo iwe ya ugali na samaki wa kukaanga sijui unapenda sana bamia au mboga za majani kama vile mchicha wa Nazi au chukuchuku kwa ugali. Pole sana kwa kukusababishia njaa.

Umenisababishia njaa.
 
Sipendi keki,tambi, ndizi za kupika,sembe,nyanya chungu,chips,kabichi,mnafu,matembele,kisamvu.

Napenda nyama sana na sijui dokta atakae nianbia nisile nyama ntamuelewaje,dona,samaki wa ziwani au maji baridi,mchicha,spinachi,matunda yote,maziwa mgando,kuku wa kienyeji tu,
 
Kaka nina kesi na wewe.
Ila kwa kutokula ugali you dont know what you are missing. Ubora wa ugali ni mbogaye bwana.

Mie namshukuru mungu hakuna nisichopenda as long as kuna nyama pembeni ila kuna nisivyokula. Hata mlenda lazma nile na nyama kama beef, kuku, samaki, kmoto and the like. Ila shida ni wale samaki wasio na sura nzuri kama octopus, calamari na wale sijui wakoje. Yaani naogopa hata kuangalia! Cha ajabu napenda prawns kama kichaa.
Mm siupendi ugali khaaaa
 
Asubuhi.
1.Uji Wa Dona Mix na Peanut Butter + Mkate wenye Peanut Butter au
2.Chai na Vitumbua au
3.Chai ya Kilk + Mkate Super Loaf au Temeke aulikuwa Coated na Mayai ya Kukaaga.

Mchana.
1.Ugali Dona + Mrenda + Samaki Sangala wasio na Mifupa(Kilo 1 wanauza Tsh 14,000/=) au
2.Wali Nazi + Maharage Nazi + Tasi wa Kukaanga au
3.Pilau Nyama + Kachumbali.

Usiku:
1.Maji tu au Juice
2.Samaki Mkavu au
3.Chai + Slace Moja.


Sipendi:
Magimbi
Choroko
Dagaa Mchele
Bilinganya
Futari ya Mihogo.
 
Back
Top Bottom