Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Vyakula nipendavyo

1)Chapati kwa maharage

2)wali za kuchanganywa bila kusahau pilau

3)pweza na seafoods wengine ispokua kaa

4)salads napenda Sana

5)kisamvu cha nazi kwa wali na mchuzi chukuchuku wa dagaa

6)muhogo wa kuchemsha na samaki wa kukaanga

7)chapati,maandazi,na vitumbu vya Nyama

8)kuku,nyama ila zaidi samaki

9)ugali samaki na kachumbari

Vyakula nsivyopenda nakula tu kwa njaa

Burger

Pizza

Vyakula vyenye sukari nyingi

Soda

Boga

Tambi
 
Napenda ndizi nyama, ndizi kuku, ndizi samaki, wali wa nazi kwa maharage na changu au nguru wa vipande alonona, biriani haswa ya nyama au kuku. Pilau si sanavya ngano napenda bokoboko haswa la kuku, mikate ya maji, ikifuatiwa na buns then mikate ya ufuta.Mayai, catles, eggchops,mtabak,msanif na mapochopocho yote yanopikwa kwa masamaki, manyama na mayai.Napenda vyakula vingi vya sukari hasa vinopikwa kwa maziwa kama pudding, faluda, custard,cheese cake, boga, mumunye, tambi, kaimati, chila, vitumbua nk.Nisije kusahau na ma pizza na ma burger, na ma hot dogs plus sandwich.Yaani mi Bulldog na napenda kula vizuri na navijua vyakula.Usije ukaniletea makande lkn wala dona, siyawezi.Byeee.
Hapo kwenye ndizi shost tutaelewana nazipenda yaani kivyovyote nazishusha dah…Lakini mimi napenda ugali ukinipa na mlenda tu japo na kipande cha nguru nitaupigaje….ukiongeza mboga ndo navimbiwa hasa samaki!!
 
Last edited by a moderator:
Jamani mimi napenda pilauuu, napenda ugali samaki pia. Ila pilau ndo usisemeeee
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mi nipe vyote lakini usininyime kitoweo
  • kuku(firigisi),nyama(moyo,maini,mafigo,utumbo),samaki,pweza,ingisi,kamba n.k

  • Napenda ndizi nyama,
  • ndizi samaki/kuku mchemsho/mafuta,
  • ndizi za utumbo/nyama za nazi,
  • muhogo wa nazi na samaki wa kukaanga,
  • Ugali na mboga tofauti kama kachumbari,mboga za majani ka mchicha/kisamvu/spinachi,mchuzi wa nazi wa samaki,mchuzi wa nyama wenye mabamia,ukauzu n.k
  • Pilau,biriyani,wali wa samaki.

  • Urojo na snacks ka sambusa,kachori,katlesi,bajia,chops,egg chop kebab n.k

  • Supu za vitoweo nilivyovitaja juu

  • Napenda salads na matunda aina tofauti

  • Vitamtam napenda ndizi mbivu za nazi,kashata,keki za aina tofauti na yoghurt ice cream
 
Mi nipe vyote lakini usininyime kitoweo(kuku(firigisi),nyama(moyo,maini,mafigo,utumbo),samaki,pweza,ingisi,kamba n.k
Napenda ndizi nyama,ndizi samaki/kuku mchemsho/mafuta,ndizi za utumbo/nyama za nazi,muhogo wa nazi na samaki wa kukaanga,Ugali na mboga tofauti kama kachumbari,mboga za majani ka mchicha/kisamvu/spinachi,mchuzi wa nazi wa samaki,mchuzi wa nyama wenye mabamia,ukauzu n.k
Pilau,biriyani,wali wa samaki.
Supu za vitoweo nilivyovitaja juu
Napenda salads na matunda aina tofauti
Vitamtam napenda kashata,keki za aina tofauti na yoghurt ice cream .

Firigisi na maini tunakula wanaume. Utaota Kipara shauri yako
 
Huyu nguru lazima awe mkavu tena wa kuchoma, au ni nguru wa vipi G? Ushabadili namba ya simu? LoL!

Hapo kwenye ndizi shost tutaelewana nazipenda yaani kivyovyote nazishusha dah…Lakini mimi napenda ugali ukinipa na mlenda tu japo na kipande cha nguru nitaupigaje….ukiongeza mboga ndo navimbiwa hasa samaki!!
 
mie ugali na sato, dagaa, roast, bamia, majani ya kunde, au mboga yoyote iliyoungwa vizuri halafu nashushia na maziwa mtindi ..... huwa najisikia niko heaven! USUKUMA NAO NI KIPAJI BANDUGU 🙂

sipendi samaki wadudu (shrimp, crabs, etc)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapo kwenye ndizi shost tutaelewana nazipenda yaani kivyovyote nazishusha dah…Lakini mimi napenda ugali ukinipa na mlenda tu japo na kipande cha nguru nitaupigaje….ukiongeza mboga ndo navimbiwa hasa samaki!!

Ndizi sio nzuri kwa wadada though
 
Back
Top Bottom