Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Mlenda umenishinda manake naona ni kama uchafu utokao puani yuckkkk!
Samahani mtakaochukia
 
matunda: papai, embe, madafu na matango aina zote
nafaka: ugali, wali na harage
vinywaji: maji, maziwa, juice ya tende
viburudisho: puding, castad
vyangu ivo apo juu
 
Hapo kwenye ndizi shost tutaelewana nazipenda yaani kivyovyote nazishusha dah…Lakini mimi napenda ugali ukinipa na mlenda tu japo na kipande cha nguru nitaupigaje….ukiongeza mboga ndo navimbiwa hasa samaki!!

Lkn kusema kweli hasa, ugali mwenzie mboga za majani. Kama mabamia na mchicha au hata cabbage la kukaanga. Mchuzi mbwembwe tu. Upate na hio kitu nguru na kakachumbari kako japo kdg. Lazim usinzie.

Mie ndizi nna asili nazo mpnz.

Si unajua mngazija kwa ndizi na utumbo?
 
Mlenda umenishinda manake naona ni kama uchafu utokao puani yuckkkk!
Samahani mtakaochukia

Mwanangu mkubwa mpe mabamia aina yoyote anakula. Anapenda bamia hatari. Na boga Na mumunye. Wakati Mi vyakula hivi nimeanza kula hivi utuuzimani
 
Lkn kusema kweli hasa,
ugali mwenzie mboga za majani. Kama mabamia na mchicha au hata cabbage
la kukaanga. Mchuzi mbwembwe tu. Upate na hio kitu nguru na kakachumbari
kako japo kdg. Lazim usinzie.

Mie ndizi nna asili nazo mpnz.

Si unajua mngazija kwa ndizi na utumbo?
apo umenkumbusha anti yangu mmoja ye hutaka utumbondizi, maana na hup utumbo uzidi
 
mi siachi asili, shelisheli napenda sana, samaki hasa changu, chapti pilau nyama, matunda napenda ispokua duriani. mkate wa kumimina sipendi na kunde au maharage ya sukari
 
mi siachi asili, shelisheli napenda sana, samaki hasa changu, chapti pilau nyama, matunda napenda ispokua duriani. mkate wa kumimina sipendi na kunde au maharage ya sukari

Shelisheli la nazi?
 
naam shelisheli la nazi na ukaliukali uwemo, nikiwa na samaki wa kukaanga pembeni, hunitoi kwenye sahani
 
Nisivyopenda choroko, mchunga, mwidu, figiri, kambale, kunde, ndizi bukoba, tambi, pizza
Ninavyovipenda sana ugali mlenda kwa samaki wa kukaanga na kachumbali, ugali daga, wali kisamvu cha karanga, wali maharage ya nazi na kachumbali, kitimoto roast, kuku wa kienyeji.
 
Nisivyopenda choroko, mchunga, mwidu, figiri, kambale, kunde, ndizi bukoba, tambi, pizza
Ninavyovipenda sana ugali mlenda kwa samaki wa kukaanga na kachumbali, ugali daga, wali kisamvu cha karanga, wali maharage ya nazi na kachumbali, kitimoto roast, kuku wa kienyeji.

Hupendi figiri?
Yaani uipate figiri changa, uikaange kwa kitunguu na mafuta tu...ule uchachuchachu wake ulie na kinyama cha kukaanga au kupande cha nguru kilichochanganywa na bamia bwasi + ugali mteke, weeeeeeeeee nakula mpaka navimbiwa.
 
Vyakula nipendavyo

1)Chapati kwa maharage

2)wali za kuchanganywa bila kusahau pilau

3)pweza na seafoods wengine ispokua kaa

4)salads napenda Sana

5)kisamvu cha nazi kwa wali na mchuzi chukuchuku wa dagaa

6)muhogo wa kuchemsha na samaki wa kukaanga

7)chapati,maandazi,na vitumbu vya Nyama

8)kuku,nyama ila zaidi samaki

9)ugali samaki na kachumbari

Vyakula nsivyopenda nakula tu kwa njaa

Burger

Pizza

Vyakula vyenye sukari nyingi

Soda

Boga

Tambi
same list except ugali samaki sipendi, ...alafu pizza napenda...
 
Mi napenda ugali rost nzito kwa maziwa mgando, wali samaki (Sato) iliyoungwa kwa nazi , wali maharage. Chapati maharage au rost, yaani ukiweza kunipikia hivyo, huna haja ya kunipa limbwata
 
napenda ndizi mshare na nyama safi isiwe ya ng'ombe wanaokula udogo na malboro, kitimoto, kuku, samaki wa ziwani, hivyo vingine nakula tu nisife njaa ila sivipendi.

hujauliza kinywaji ndio maana sijasema napenda kinywaji gani.
 
napenda vingi,but chips sekela,calamari na mashed potatoes tops my list...
sijui sipendi chakula gani mana am quite a food lover ambae sinenepi kirahisi,labda korosho znanikinaisha nikila hata pc mbili
 
Back
Top Bottom