Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

mimi nachukia sana ugali wa sembe,pilau,wali,chips,nyama,chai yenye sukari na vyakula vyote vilivyokaangwa
 
sipendi nyanya chungu,bilinganya na vitunguu maji, hasa vitunguu ukiviapply kwenye maharage au nyama afu nivione vikielea wee!
 
sikupendi ugali!!!!sikupendi sikupendi tena sikupendi!!!!!dah ila ndo umenikuza wewe
 
vyakula vyangu nnavovipenda
1: wali na aina zote za wali pilau, biriani
2: mboga zote isipokua mlenda
3: mikate yangu nnayopenda ni chapati, mkate wa mayai na maandazi
4: napenda supu ya pweza na ya nyama ya ng'ombe
5: napenda sana maziwa ya ng'ombe
6: napenda urojo
7: napenda juice ya muwa, ya pension na juice ya kerot
8: matunda, hapa napenda tikiti maji, nanasi, embe na papai
 
Magimbi,mseto,dona,mihogo ya kuchemsha,lozi,karanga mbichi,chapati zilizopikwa kwa samli,samaki,maziwa,mayai ya kienyeji,asali,mkate wa kahawia pamoja na matunda yote na mboga za majani ndivyo vitu nivyovipenda.
 
Back
Top Bottom