Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Napenda mboga za majani, vyakula vyenye madini chuma na matunda
 
Mi sipendi wali maharage, ugali maharage, Napenda sana ndizi nyama na ndizi samaki lakini sio ndizi wa kilimanjaro
 
Napenda ugali dagaa samaki kuku kisamvu matembele figiri mlenda maharage ila nile na ugali dagaa au nile na wali AU na Ugali na samaki wa kukaanga na mboga ya majani. Sipend Makande ndizi viazi mbatata majani ya kunde
 
Napenda: Ndizi-nyama (mshale mgumu), wali, pasta, chapati maji na za kawaida, vitumbua, matunda, mboga mboga kwa sana tena spinach, mtindi, zege, rolex ya Uganda, nyama ya kuku na ya kanga, kachumbari, samaki wa salmon, johari na sato vilevile matunda karibia yote.

Aste aste: Ugali, pilau, nyama ya ng'ombe - naupenda na siupendi hivyo nakula mara chache.

Sipendi: Makande, dona, biryani, mihogo, uyoga, mlenda, maharage, supu, viazi vya kupikwa, nyanya chungu, uji.

Sili kabisa: nyama ya utumbo, mbuzi & kondoo, prawn, shrimp, crab, mussel, lobster, kisusio.
 
Jalapeños ni kama pili pili lakini unaweza kuweka
Kwenye sandwiches au kupikia zina harufu
Tamu kweli.

images
Juzi juzi nilinunua Pringles za jalapeño. Nzuri sana kwa kweli.
 
Ndizi mzuzu iliyoiva vzr ichomwe, ichemshwe au ikaangwe napenda sana, kinyume ndizi mbichi mzuzu
 
Napenda vyakula vyote isipokua;
1.kitimoto(kutokana na Imani yangu ya dini)
2.Majani ya Kunde
3.Mnafu
 
Napenda sana kula vyakula jamii ya ngano kama;

1. Chapati

2. Maandazi

3. Half cakes

4.Tambi

5.Napenda mboga kama maharage, samaki sato, mchuzi mzito wa kuku

6.Napenda nyama ya kuku

7.Samaki au kitimoto

8.Nyama za aina nyingine si mpenzi nazo sana

9. Napenda sana juice ya mananasi au maembe

10.Napenda matunda kama ndizi, parachichi au papai.

Vyakula nisivyovipenda;

1.Makande

2.Dagaa

3.Maziwa mtindi

4.Mihogo ya kuchemsha

5.Dona

6.Mikate

7.Bamia

8.Matango

9.Pilipili ya aina yeyote

10.Nyanya chungu

Yaani vyakula ambavyo hupendi mie ndo napenda kasoro mkate toa siutaki kabisa
 
Napenda Wali na bamia - (bamia likatwe dogo dogo litiwe na nyanya chungu)
 
Back
Top Bottom