Tetesi: Chalamila adaiwa kuhusika na ufutaji wa kipindi Wasafi FM

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Dakika chache baada ya waziri Nape kukanusha kuwa serikali ya rais Samia haihusiki na kukifuta kipindi cha mahojiano kilichopaswa kuruka leo asubuhi pale Wasafi FM, kuna tetesi kuwa Chalamila anahusika.

Habari kutoka ndani ya Wasafi Media zinadai RC Chalamila ndiye aliyewapigia simu majira ya jioni kuwataka kukifuta kipindi hicho. Na ndipo nao Wasafi Media jana usiku wakampigia Tundu Lisu.

Ikumbukwe Chalamila ndiye aliyetaka kuzima hata maandamano ya chadema ya 24 January 2024 kwa kisingizio kuwa jeshi litakuwa linafanya usafi.

Swali. Kama tetesi hizi ni za kweli. Je, Chalamila siyo sehemu ya serikali ya Samia?
 
Hizo ni promo za kituo cha ma-vilaza tu, Serekali iko clear, kama iliruhusu maandamano, haiwezi kuzuia maongezi ya kwenye redio. After all nani anayesikiliza redio siku hizi tena hiyo radio ya ki-pimbi
 
TV chadema iko mfukoni kwa Mwenyekiti wenu?
 
Serikali itoe kibali cha maandamano plus mikutano halafu wazuie interview...Mbona mnaaminishwa mambo ya kipumbavu.

Hao wote ni wanasiasa tafuteni kazi za kufanya.
 
Kila mtu ana tetesi zake. Twitter republic wanasema Nape. Maana ndio tabia yake ya siku nyingi kupigia wenye Tv, Radio na online tv kuzuia wapinzani wasioneshwe wala kusikika.
Ni kweli. Awali ilivuma kuwa Nape ndiye kawapogia simu, lkn sasa kakanusha.

Na ndiyo maana tetesi zimehamia kwa Chalamila hivi sasa
 


Who cares?
 
Tetesi za huku mtaani ni kuwa Mbowe ndio ametaka makamu mwenyekiti anyimwe air time sababu hawajajua anataka kuzungumza nini!
 
Ni kweli. Awali ilivuma kuwa Nape ndiye kawapogia simu, lkn sasa kakanusha.

Na ndiyo maana tetesi zimehamia kwa Chalamila hivi sasa
kwahiyo na Chalamila akikanusha, jumba anaangushiwa mwengine ama vipi?
 
Who is Chalamila kwenye hili Taifa letu?🤬🤬🤬🤬
 
Chalamila ni mwendawazimu Tu ndio maana anatumia majukwaa ya Serikali ku-promote hotel ya Ndugu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…