Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kitendo alichofanyiwa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo, ni kinyume cha sheria na maadili ya Mtanzania.
Amesema binti huyo kwa sasa yupo kwenye mikono salama ndani ya moja ya vituo vya mkoa wake, akipata elimu ya unasihi itakayomsaidia kujikuza katika maisha yake ya kila siku.
Chalamila amesema hayo jana Agosti 8, 2024 akizungumza na Mwananchi ikiwa ni siku nne zimepita tangu Agosti 4, ziliposambaa picha jongefu kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu wakimtaka kumuomba radhi mtu waliyemwita kwa jina la ‘afande’.
Soma Pia:

- Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu
- TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam
- LHRC walaani vikali tukio unyanyasaji wa kijinsia linalodaiwa kutokea Temeke