- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Mtumiaji mmoja wa Instagram alichapisha kipande cha video kinachomuonesha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na kuambatana na ujumbe unaosomeka kwenye grafiki "KILE KITUO CHA MAFUTA NI CHA MTOTO WA SAMIA". Tazama hapa
Kwenye kipande hiko cha video Chalamila anasikika akisema;
"Hiki kituo cha mafuta mnachokiona hapa ni cha mtoto wa Rais"
Uhalisia wa video hiyo ni upi?
Baada ya ufuatiliaji wa JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo imehaririwa kutoka katika video halisi na hivyo kupoteza uhalisia uliokusudiwa.
Kipande hicho kimehaririwa kutoka katika sehemu ya hotuba aliyoitua Chalamila Juni 5, 2025 wakati wa kilele cha harambee ya kuchangia kituo cha watoto wenye mahatijai maalumu cha Bagamoyo Diaconic Lutheran. Tazama hapa na hapa
Ambapo Chalamila aligusia kuwa kumekuwa na watu wenye hulka ya kuwazushiwa ama kuoa taarifa sahihi kuhusu umiliki wa mali mbalimbali wakihusisha Marais na watoto wao na ndipo alipotelea mfano wa mtu mmoja aliyekuatana naye na kumueleza kuwa kituo fulani cha mafuta ni cha mtoto wa Rais.
Chalamila alisema;
"Ambacho leo nimeona nikiseme kwa sababu niko kwenye madhabahu haya muhimu sana. Siku chache zilizopita mheshimiwa Rais mimi nilikuwa nafanya mazoezi nikakutana na kijana mmoja aliyeamua kunisimulia makubwa ambayo mimi sikuwa na uhakika nayo.
Wakati niko nafanya mazoezi yule kijana akaniambia mheshimiwa Chalamila hiki kituo cha mafuta unachokiona hiki ni cha mtoto wa Rais nikamuuliza Rais gani akasema Rais Samia nikamuuliza mtoto yupi huyo akamtaja jina nikamuuliza una uhakika akasema haki ya Mungu nina uhakika jana alikuja mwenyewe kulipa pesa kwenye kituo hiki na nilimuona mwenyewe kabisa na tukasalimiana"
Hivyo kipande hicho kinachosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kinapotosha uhalisia kutoka katika video halisi na si cha mwaka 2026.