Chalamila amesema wafanyabiashara wako wa aina kadhaa ikiwemo walioshiba, kati na wachanga na iwapo wataigana kuna watakaojuta leo, kesho na mwingine baaada ya mwezi mmoja. Chalamila amesema ni kweli wafanyabiashara wanaweza kuwa na changamoto lakini zipo nyingine za kisheria na haiwezaki kuzisuluhisha asubuhi na mapema.
Chalamila amesema duka si sawa na hospitali kwani hospitali zingegoma ingekuwa hatari zaidi na kuomba busara itumike. Mwisho amemaliza na mkwara mzito kwa yeyote atakaempiga mkwara aliyekubali kufungua.
"Aliyekubali kufungua afungue na yule ambae atamletea mkwara mtu yeyote yule aliyekubali kufungua naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonesha shoo nzima. Wewe unakuja unamletea mkwara, mimi nitakuchimba mkwara na hautaamka tena, na hili naomba niwaeleze ndugu zangu wa Kariakoo, utoto ukizidi hatuwezi kufikia hapo"
Pia Chalamila amewashukuru waliofungua maduka na kuwaahidi waliofunga atazilinda biashara zao na hakuna mwizi atakaeiba hata kama itakuwa mwezi. Chalamila amesema biashara sio siasa na leo jioni wataona hasara yake lakini siasa haiwezekani kugundua hasara zake.
Chalamila pia amedai yeye kama mkuu wa mkuu wa mkoa akiumua kwenda kukaa madukani kwao aangalie kiwango kikubwa cha ukwepaji kodi, amehoji kama wataweza kuishi Kariakoo!
We mtu amevimba tumbo na mwili, amekaa kwenye kiti cha kuzunguka masaa 10 j3 hadi ijumaa tu na anapigwa AC asubuh hadi.jioni kushika.shika.mafaili tu na simu basi, anajua nini kuhusu hustle za mfanya biashara?
We utakuwa mjinga sana na hujui chochote,na ujinga kama wako ndiyo wanasiasa wanautumia,kama unawatoto wanakuita Baba basi wana Baba wa ovyo kabisa kuwahi kutokea duniani.Acha kukurupuka wewe na ukoo wako mnaathirika na mfumuko wa bei ya bidhaa acha ubwege