Chalamila, badala ya kuzunguka Mkoa wa Kagera ukilalamika na kuzogoa, tafuta Suluhu, vinginevyo wapinzani unawapa njia, shirikiana ujue tatizo

Chalamila, badala ya kuzunguka Mkoa wa Kagera ukilalamika na kuzogoa, tafuta Suluhu, vinginevyo wapinzani unawapa njia, shirikiana ujue tatizo

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, anacheza blame game. Kwa kagera hii itamtoa nje ya mchezo.

Ni kweli Mkoa una changamoto, namshauri akae na wadau wa Mkoa. Waone mikakati na mbinu za kuukomboa Mkoa. Muda anaotumia kushambulia na kulalamika, hautasaidia lolote.

Kahawa imekufa, sawa, lakini kina zao la vanilla, tunataka aongelee hili pamoja na MASOKO yake. Amwite Bashe wajadili.

Juzi tu hapa Wizara ya Kilimo iliweka zao jipya la kimkakati, michikichi, natarajia mkuu wa Mkoa baada ya muda mrefu, amualike Samia na kuonyesha Malaki ya hekta za michikichi na kiwanda Cha kukamua mafuta kilichojengwa, na mkakati wa kununua chikichi hizo. Na pia aweke mkakati, Kila kaya iwe na chikichi zisizopungua tano, na kwenye shamba, walau 20.

Kuna beach nzuri sana kagera, utalii anaujadili vipi? Ameomba kisiwa hata kimoja Jiwe maalum kwa utalii kagera? Kuna msila pale.

Zao la ndizi, ana mkakati gani wa kuipeleka ndizi ya kagera soko la kimataifa?

Aina ya uongozi anaotumia ni WA kufoka foka, kulaumu. Je anajua Kuna chuo Cha kilimo Maruku? Ana engage nacho vipi kuikomboa kagera?

Anashirikia na viongozi wa dini kufuatilia vyuo vikuu vilivyofungwa vifungukiwe?

Anaibadili vipi mtukula upande wa Tanzania iwe na hadhi na kuvuta wafanyabiashara?

Bashiru na akina mwijage amekaa nao? Hao walikaa na Mh. Samia wakajadili changamoto za kagera.

Taa za barabarani, ikifika usiku mji una Giza kama kuzimu.

Soko la Bunazi, na mengine mengi.

Anafuatilid suala la stendi? Soko?

Tunahutaju a-engage, wadau wapo
 
Akili za kizuzu hizi zilizoviringishwa kwenye uzumbukuku pamoja na ujinga uliopakwa unafiki. Kwani wapinzani ni maadui wa nchi hii?
Hoja yake nzuri sana ila kwa bahati mbaya sana kaitia makorokoro ya "Wapinzani unawapa njia". chiembe huo ushauri uliotoa Chalamila anaweza kuutekeleza na watakaofaidika ni wananchi wa Kagera na wala si wana CCM au wapinzani wa CCM pekee.

Haya Makorokoro ya kudhani kila jambo lifanyike ili wengine wasipate njia, ni ujinga uliotujaa na inatupasa tuutoe.
 
Kilio cha wana kagera ni stendi..jamaa hawana stendi kabisa
 
Chalamila yupo sahihi ukombozi wa fikra ndio muhimu kwanza kabla ya yote.wahaya mubadilike.muache ugoloko
 
Hivi Bukoba Imekosa Wazee ?

Wanasiasa wanakuja wanatukana watu wanaondoka, mmekaa kimya, tena katika nyakati ngumu kama tetemeko la ardhi.

Si chama chake, Serikali wala familia yake inaomba radhi kwa matusi yale mazito
Halafu anateuliwa mwingine bado na yeye anakuja na sera zile zile za matusi baada ya kukaa na Wadau wa Maendeleo

Wazee, Wasomi, Wazawa wa mkoa wa Kagera mmekuwa maboya kiasi hiki ?

Siamini ninachokiona kabisa nilidhani ziara ya SSH Kagera pamoja na mengine yote basi kwa niaba ya CCM/Serikali ya JMT angeomba radhi Wananchi wa Kagera kwa matusi yaliyovurumishwa na mtangulizi wake, aidha angeenda mbali zaidi na kukiweka mbali chama/serikali yake kwamba utamaduni wa matusi sio wao, cha ajabu anateuliwa RC naye anakuja na Sera zilezile za matusi

Hii hali isipodhibitiwa heshima ya watu wa Kagera itapotea
 
Kazi wanafanya na ndiyo maana maisha yao yanaendelea. Labda hawajali mambo ya Umma. Kagera wanajiendeleza kibinafsi. Utakuta mtu kajenga bonge la nyumba migombani lakini hakuna barabara ya maana inayokwenda huko.
Mkoa uko mkiani afu unasema wameendwlea?
 
Ujuaji wa wajaya na uvivu.....😂😂😂 kuna sehemu kule katoro kunaitwa buselesele haisee hii sehemu wahaya wamejaa na ukijichanganya ukampa dili muhaya hakuna litakalofanyika zaidi ya kuongea sana kama chiriku....eti chonka kyomaa mbwenu 😁😁😁😁😁
 
Hivi Bukoba Imekosa Wazee ?
Wanasiasa wanakuja wanatukana watu wanaondoka, mmekaa kimya, tena katika nyakati ngumu kama tetemeko la ardhi
Si chama chake, Serikali wala familia yake inaomba radhi kwa matusi yale mazito
Halafu anateuliwa mwingine bado na yeye anakuja na sera zile zile za matusi baada ya kukaa na Wadau wa Maendeleo

Wazee, Wasomi, Wazawa wa mkoa wa Kagera mmekuwa maboya kiasi hiki ?

Siamini ninachokiona kabisa nilidhani ziara ya SSH Kagera pamoja na mengine yote basi kwa niaba ya CCM/Serikali ya JMT angeomba radhi Wananchi wa Kagera kwa matusi yaliyovurumishwa na mtangulizi wake, aidha angeenda mbali zaidi na kukiweka mbali chama/serikali yake kwamba utamaduni wa matusi sio wao, cha ajabu anateuliwa RC naye anakuja na Sera zilezile za matusi

Hii hali isipodhibitiwa heshima ya watu wa Kagera itapotea
Wazee wa Kagera washirikishe watani wa Kigoma wapewe kitu TOKA Ziwa Tanganyika, ili waanze kumtia adabu Chalamila,

Wazee mpo undeni kamati, mshirikisheni na mtani wenu Makam wa Rais , si ni mtani wenu TOKA Kigoma ,mnakwama wapi?
 
Mimi wahaya nawafahamu sana bro akiwa na mkungu wa ndizi ndani na balance kidogo ya fedha humuambii kitu....
Hiyo ni Life style yao. Na makabila mengi chakula ndiyo kila kitu. Ndiyo maana hata salamu zetu za asili huwa tunaulizana "umekula nini"?
 
Chalamila ameanza kuwaumbua wahaya kwa umasikini uchawi uvivu na uzinzi ktk mkoa wao, sasa wameanza kulialia na kumsema mitandaoni... Tulieni vilaza nyie mwanaume huyo awasaidie kuwafumbua akili... Mkoa upo upo kama dampo lililo telekezwa
 
Mimi wahaya nawafahamu sana bro akiwa na mkungu wa ndizi ndani na balance kidogo ya fedha humuambii kitu....
Ila tukubali mkuu Kagera Kama leo ukasema migomba wafyeke Yani pawe wazi , tutakutana na jiji jipya lililokua limejificha kwenye migomba,

Huko Migombani wajomba wamepiga vitu sio vya kitoto, ALAFU utakuta wanaishi wazazi , ndugu, na wakati mwingine mfanyakazi wahusika wopo Mikoa mingine wanapambana na Maisha,

Tuliendaga msiba mmoja sikumbuki ni Kijiji gani e BWANA unakutana na kitu katikati ya Migomba, unalinganisha na mtaa unapoishi mikoani, hupati jibu, hacha wajidai bwana makwao wanapatendea haki aisee
 
Wahaya wamekataa kufyeka Migomba yoa. Lakini siyo kweli kwamba hawajaendelea. Idadi yao pia siyo kubwa sana ukilinganisha na eneo walilonalo.
 
Back
Top Bottom