Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam hana akili timamu. Huwezi kumtofautisha na yule aliyewahi kusema wasioweza kulipa 200 pale kivukoni wapige mbizi kuvuka.Na watoto wetu wachanga uji tuwapikie na nini? Nao tuwaambie sukari ina madhara?
Upuuzi mwingine bwana.
Professor Janabi ni vizuri ajikite kuendesha semina Kwa wagonjwa ambao maradhi wakiyonayo Wala hayakutokana na utumiaji Sukari,chumvi,Wanga ,nyama au Mafuta Lakini tiba Yao inahitaji waache hivyo vituMkuu wa mkoa wa Dar es salaam hana akili timamu. Huwezi kumtofautisha na yule aliyewahi kusema wasioweza kulipa 200 pale kivukoni wapige mbizi kuvuka.
Huyu jamaa sometimes sijui huwa anatumia akili za wapi kufikiria!Chalamila asema ukimsikiliza Dr. Janabi anasema ulaji wa sukari nyingi unasababisha maradhi mengi, kwahiyo wakati huu ambako sukari imeadimika tuachane nayo kabisa ili usiweze kupata matatizo ya afya hapo baadaye.
Kwahiyo serikali imeshindwa kabisa kutatua changamoto hii ya upatikaji wa sukari sasa wanatafuta 'justification' ya ukosefu huo?
Bashe ilibidi uwajibike kwa kushindwa kutatua hili hadi hali imekuwa mbaya hivi.
Pamoja na haya yote bado viongozi mnakula kwa kama zenu na hutasikia posho za wabunge zimepungua, ama wamechukua 'initiatives' za kubana matumizi ili kupunguza makali haya kwa wananchi.
Bure kabisa!
Sasa kwa muonekano wa huyo Prof je kweli ni mwenye afya? pamoja na kushindia mchicha anaonekana mgonjwa tu.Wakati Changamoto ya uhaba wa sukari ikizidi kushika Kasi, viongozi wamekuwa wakinukuliwa kusema watu waachane na matumizi ya Sukari Kwa sababu sio salama kiafya kama ambavyo Mkuu wa Mkoa wa Dar Albert Chalamila amenukuliwa.
Hii ni Kauli ya pili ,ya kwanza ilitoka Kwa Prof.Janabi na kuungwa mkono na Waziri wa Afya.
Swali.Je huu ndio msimamo wa Serikali au msimamo binafsi wa Chalamila na wengine?
RC wetu anajua sukari ni kunywa chai tu, hajui kuna dawa zinatengenezwa kwa sukari. Kuna viwanda vya vinywaji n.k..viongozi wetu hawajali.
..na ukweli huo unajidhihirisha ktk kauli kama iliyotolewa na RC Chalamila.
..kodi zetu zinatumika kulipa mishahara ya viongozi wanaotukejeli.