Chalamila: Kuna vijana wanataka kuchoma bandari kavu, kisa foleni

Chalamila: Kuna vijana wanataka kuchoma bandari kavu, kisa foleni

Siyo mbaya ila haiwezi kuungua kwa sababu ina maji.
Hivi Chalamila hajui kuwa serikali ilihamishia Kwala bandari kavu zote na ikaweka treni ya SGR kupeleka huko makontena, sasa wanang'ang'ania nini Dar!

Badala yake wanajaza malori mjini. Eboo.
Kurasini na Kigamboni hakuendeki
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefanya kikao na viongozi wa mkoa huo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya foleni katika jiji hilo.

Akizungumza ameeleza kuwa foleni imekuwa mwiba na miongoni mwa visababishi imekuwa ni bandari kavu ambazo zipo katika makazi ya watu hasa Kigamboni.

Chalamila ameeleza kuwa amepata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna vijana wamejipanga kwenda kuchoma moja ya bandari kavu kwa sababu inasababisha foleni katika maeneo wanayoishi.

We Mzee Chalamila si ni hivi majuzi tu ulisema— "vikorola vyetu namba A, vichafu chafu na visiyo na air condition"— ndiyo vinasababisha foleni jiji la Saridalam?
 
Unajibu kwa mihemuko badala ya kujibu hoja za kiongozi wa Mkoa, jambo linaloonyesha upungufu mkubwa wa uwezo wako wa kuchambua masuala kwa mantiki. Ulichokiandika kimeweka wazi kiwango chako cha uelewa na namna unavyoshindwa kutofautisha hoja na hisia.
Viongozi gani hapo au wababaishaji tu kama wewe hapo...!?Mfumo wote wa Uongozi umeshafeli,Nchi inajiendea tu.R.C.na Mawaziri wanakuwa wa kwanza kupata taarifa za Kiintelejensia na kuzitoa kwa UMMA huku Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama hawajui lolote.!!Amri ya kutolewa na Rais nayo inatolewa na Waziri au RPC.!??
 
Kwani wewe unajuwa job description ya RC? Kama hujui nitakujuza
 
Kwani wewe unajuwa job description ya RC? Kama hujui nitakujuza
Huna unalojua zaidi ya kujikomba:RPC-Dar:Marufuku kutoka nje-29.10.2025,Katambi-Marufuku Mikutano ya Vyama vya Siasa,Rahisi Samia- Hatutazuia tena Mikutano ya Vyama vya Siasa wala Maandamano,RPC-Dar-Jiji liko salama Wananchi endeleeni na Shughuli zenu,P.M- Vijana wamelipwa waandamane na wengine wa kutoka nje wameingia....Uharo ni mwingi tu.
 
Chalamila kanipa mbinu ya kuwaadabisha hawa madikteta wa awamu ya sita.Ni mwenda kuchoma tu bandari kavu ili wasikilize matakwa yetu ya kuacha kuteka hovyo watu wetu kama polepole
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefanya kikao na viongozi wa mkoa huo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya foleni katika jiji hilo.

Akizungumza ameeleza kuwa foleni imekuwa mwiba na miongoni mwa visababishi imekuwa ni bandari kavu ambazo zipo katika makazi ya watu hasa Kigamboni.

Chalamila ameeleza kuwa amepata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna vijana wamejipanga kwenda kuchoma moja ya bandari kavu kwa sababu inasababisha foleni katika maeneo wanayoishi.

Kwani si kuna mtu alipewa milion kumi kwa kuwa aliweza kubuni suluhu ya kuondoa foleni.
Hii nchi hii
 
Hawa viongozi wenu ni waongo waongo tu. Mwigulu nae kaongopa vijana wamekatwa na mabomu, sasa wako wapi? Mbona hawaonekani kwenye taarifa ya habari?
 
Back
Top Bottom