Chalamila: Machinga aliyepewa fremu mwisho miaka mitano, baada ya hapo nakufukuza

Chalamila: Machinga aliyepewa fremu mwisho miaka mitano, baada ya hapo nakufukuza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wafanyabiashara ndogo maarufu kama Machinga kutumia fursa wanazopata kujiendeleza na kuachana na biashara ndogo, akisema lengo ni kuwawezesha kukua hadi kuwa wafanyabiashara wakubwa na walipakodi.

Akizungumza leo, Oktoba 7, 2026, wakati wa ziara yake ya kuwatembelea Machinga wanaopangwa katika Kata ya Msigani, Mbezi Chalamila amesema Serikali haiwezi kuendelea na utaratibu wa kupanga Machinga kila siku bila kuweka mpango wa kuwawezesha kukua kiuchumi.

“Leo wewe ni Machinga, lakini tunategemea baada ya miaka mitatu, minne uendelee kuwa mfanyabiashara wa kati na baadaye mfanyabiashara mkubwa, ili uweze kulipa kodi ya Taifa,” amesema Chalamila.

Amesema Machinga wanaofanya biashara Kariakoo wamepewa hadi Oktoba 24, 2026 kuondoka katika maeneo yasiyoruhusiwa, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kuweka utaratibu mzuri wa biashara jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Msigani, Zaidi Murilo amesema wafanyabiashara hao wanahitaji zaidi kupewa vibanda ili waweze kuendesha biashara zao katika mazingira rasmi, jambo ambalo pia litawezesha Serikali kupata mapato.
Murilo ameishukuru Serikali kwa kuweka mpango wa kuwatafutia machinga maeneo ya kufanyia biashara na kuwaweka katika maeneo hayo bila usumbufu.
#Video
 
Mji hauwezi kosa machinga, Chalamila hajui anachoongea.

Hata kama machinga wa leo baada ya muda mitaji yao ikikua wakaanza kulipa kodi kama anavyotaka, bado watazaliwa machinga wengine.

Watazaliwa wengine kwasababu machinga ni matokeo ya mitaji midogo, na hili so kosa la machinga.

Ni kosa la serikali iliyoshindwa kuweka mazingira mazuri ya kutoa mikopo kwa machinga ili wazimudu biashara zao mapema.

Ile mikopo wanayotoa kwenye halmashauri imekaa kiupendeleo, machinga asipokuwa na muonekano wa kiCCM hapewi.
 
Wewe ndo hujamuelewa chalamila, kamsikilize upya
 
Wewe ndo hujamuelewa chalamila, kamsikilize upya
Nirudie kumsikiliza vioi ikiwa ameshakosea toka mwanzo.

Machinga kuwafukuza mijini sio mara ya kwanza, huwa wanafanya hivyo kila mara.

Wanatakiwa wajiulize kwanini tatizo haliishi. Kuwafukuza mijini ni sawa na kuficha tatizo, sio kulimaliza.

Wakimaliza la mitaji, bado kuna maeneo ya kufanyia biashara, hayo maeneo waliyoyatenga kwa machinga hayatoshi ukilinganisha na idadi na machinga waliopo na wanaoongezeka kila siku toka mikoani.
 
Mipango miji ndio tatizo kubwa
Miji mikubwa duniani wauzaji wadogo wapo ila kuna sehemu ziliachwa makusudi kwa ajili hiyo na sio pengine bali ni kwenye mkusanyiko wa watu

Tatizo linakuja ni hapo Kariakoo hakuna mahali wanapoweza kuwekwa zaidi ya kuwaondoa kwa sababu hakuna nafasi
 
Back
Top Bottom