Chalamila: Mtoa huduma wa mabasi ya mwendokasi Kimara tunamsimamisha

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert John Chalamila, leo amefanya ziara katika kituo cha mabasi ya mwendokasi kilichopo Kimara Mwisho na kuzungumza na wananchi kuhusu changamoto ya upungufu wa mabasi. Katika ziara hiyo, Mhe. Chalamila amesema serikali inatambua changamoto hiyo na tayari imechukua hatua madhubuti kwa kuagiza mabasi zaidi ya 200 ili kuboresha huduma.
Alibainisha kuwa mabasi hayo yanatarajiwa kuwasili nchini ndani ya wiki hii na mara yatakapofika yataanza kazi mara moja ili kupunguza msongamano na kero zinazowakabili wananchi wa jiji la Dar es Salaam. Aidha, Chalamila ameongeza kuwa mtoa huduma wa sasa katika njia ya Kimara ataondolewa mara moja baada ya mabasi hayo mapya kuwasili, na tenda hiyo itakabidhiwa kwa mtoa huduma mwingine mwenye uwezo wa kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa amewahakikishia wakazi wa jiji hilo kuwa serikali itaendelea kuboresha huduma za usafiri wa umma kwa kuhakikisha upatikanaji wa mabasi ya kutosha na kuimarisha mfumo wa mwendokasi kwa maslahi ya wananchi wote.
 
Huyu jamaa naye ni Chalie!
Aligundua lini kwamba mabasi 200 yanahitajika?
Transpostation ni business isiyotaka mikurupuko na maamuzi ya juu juu.
Wateja wapo miaka yote, mradi unakurupuka sasa, alikwiii!!
 
Kwahio kosa lilikuwa ni mtoa Huduma, au hao ambao walijua kwamba magari hayatoshi hadi kuagiza mengine 200 ?

Kama ndivyo baada ya kumsimamisha huyo kazi ajiondoe yeye pamoja na kumshauri boss wake pia; Mimi kama Mlipa Kodi ninayewalipa wote ninachelea kusema wote kazi imewashinda...
 
Back
Top Bottom