GE2025 Chalamila: Mwendokasi umepoteza Ladha, mtu mwenye tai hawezi tena kupanda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, amesema upungufu na kutokuboreshwa kwa Mabasi ya Mwendokasi ni vitendo vya kuwahujumu Wananchi wanaotumia usafiri huo ni hujuma dhidi ya juhudi za serikali hususan katika kuleta maendeleo na kuwahudumia Wananchi.

Akiwa Kituoni hapo asubuhi ya leo Julai 24, 2025, katika ziara kwenye Kituo cha Mwendokasi Kimara Mwisho kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu upungufu wa Mabasi hayo, Chalamila amesema hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na kuonya kuwa serikali haiwezi kuvumilia uzembe huo unaojirudia kila mara.

Chalamila amesema tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo takribani miaka Tisa iliyopita, hakuna jitihada zozote zilizochukuliwa kuboresha au kuongeza Mabasi, hali inayosababisha msongamano na kuchelewesha safari za Wananchi.

Mkuu wa Mkoa pia amehoji ni kwa namna gani mtu binafsi anaweza kutumia gari moja kwa miaka tisa mfululizo bila kufikiria kulibadilisha, achilia mbali magari ya umma yanayohudumia maelfu ya Watanzania kila siku.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameonya kuwa kama wahusika wa usimamizi wa huduma hiyo hawatabadilika na kuchukua hatua madhubuti mara moja, basi atapendekeza wachukuliwe hatua kali, ikiwemo kuondolewa kwenye nyadhifa zao.
 
Iko siku huyu jamaa atapigwa na kopo za mikojo na hiyo siku haiko mbali.
 
binafsi kuna jambo nashindwa kuelewa, hivi ni kwa nini huyo mkuu wa mkoa hasimamii watu wapande kwa foleni badala ya kupigania na kupitia madirishani? kwa nini wasipange foleni na aliyefika kwanza ndiyo apande kwanza ? polisi wanaweza kulisimamia hili, hata kama mabasi hayatoshi bado watu wanaweza kuwa wastaarabu.

jamii ambayo mwenye mabavu ndiyo anaishi ni jamii ya masokwe porini …
1753349781703.jpeg
 
View attachment 3416620
Kwa jinsi hali ilivyo sasa swala la kupanga foleni haiwezekani.

Wakisema abiria wapange foleni , foleni zitakuwa ndefu sana. Tena zitatoka hadi nje ya kituo, maana watu ni wengi na gari ni chache,
Na watu wakijaa kituoni si rahisi utaratibu wa foleni kuendelea.

KAma mwezi mmoja umepita pale kivukoni kulikuwa na askari ana simamia foleni,
Kuna siku watu walijaa gari ilipokuja abiria wakaingia kwa fujo, askari alikuwa anazuia walipita nae ndani.

Dawa ni kuleta mabasi.
 
Back
Top Bottom