Chalamila na Janabi acheni kutafuta Kick kwenye Maisha ya watu

Chalamila na Janabi acheni kutafuta Kick kwenye Maisha ya watu

Umewashambulia bila sababu, Janabi ni mtaalam wa afya hivyo uwepo wake una umuhimu, Chalamila ni RC ni vizuri pia akiwepo kuonesha uwajibikaji
Hapo hahitajiki Profesa mtaalam wa afya. Wanaohitajika ni wataalam wa uokoaji na watu wa huduma ya kwanza. Profesa anapaswa kukaa hospitali ili kujiandaa kupokea majeruhi kwa kuhakikisha theater ziko tayari, damu ipo ya kutosha. Aidha kuhakikisha madaktari, manesi na mafundi mchundo wako standby kuhudumia wagonjwa.

Hapo yeye na Chalamila wanaingilia juhudi za kuokoa maisha ya watu kwa kuwa wao ndio centre of attention kuliko majeruhi.

Amandla...
 
Mleta uzi kuna vitu vingine vichukulie positive tu. Unataka janabi awepo kana kwamba hapo hapawezi kuwa na majeruhi anayehitaji msaada wa haraka. Chalamila ni Mkuu wa Mkoa lazima awepo
Washike Koleo na wao
Huyo mwingine tumbo kubwa tu

Ova
 
Mwenye Jengo naye kafa? Mkome mmezoea kila kitu porojo tu, utakuta hapo watalaam walitoa angalizo, rushwa ikapita mwanaharamu akafunika kombe maisha yakasonga, Sasa haya ndio madhara ya joint expansion.

Inaonekana watu hawana Hela ila wanalazimisha kujenga magengo marefu Kwa kutumia budget kiduchu na engineers Michael aka uchwara.
Hatar sana !
 
Umewashambulia bila sababu, Janabi ni mtaalam wa afya hivyo uwepo wake una umuhimu, Chalamila ni RC ni vizuri pia akiwepo kuonesha uwajibikaji
Wendawazimu. Janabi anachofanya ni nini hapo? Utaalamu wake ni upi ambao una msaada hapo?
 
Mleta uzi kuna vitu vingine vichukulie positive tu. Unataka janabi awepo kana kwamba hapo hapawezi kuwa na majeruhi anayehitaji msaada wa haraka. Chalamila ni Mkuu wa Mkoa lazima awepo hapo.
JANABI NI DR WA NINI? HAPO ANASAIDIA MAJERUHI GANI? TUACHE KUFANYA MZAHA NA SIASA
 
Nje ya mada hiyo ghorofa iliyoanguka Ina floor ngapi na Ina muda Gani au ni pagala
 
Zimamamoto wako wapi ??? Kazi yao kupita kwenye majengo na kukushanya ushuru wa moto na uokoaji lakini IKITOKEA KAMA HIVI HUWAONI ??????!!!!
 
Winchi ya kunyanyua vifusi inafungwa sehemu gani kwenye greda? Au we ndo wale kila mtambo mnaita greda?
Haaaaa yy anajua great tu kimbembe liletwe anasema kumbe dio grader tz ushamba umewazidi vitu vidg hawavijui hahaa
 
Hapa Kariakoo jengo limeanguka. Hakuna vitendea kazi Chalamila na Janabi wamefika kupiga stories.

Muda mrefu linahitajika greda kuja saidia kuinua nguzo nzito. Vifaa vya kuekolea hamna. Anakuja Mkuu wa Mkoa na Dr. Janabi eti kuokoa? Wanaokoa nini kama si kutafuta kick na attention kwa watu?

Huyu Janabi angefanya jambo la maana kuhakikisha kule Muhimbili kila majeruhi anayefikishwa anashughulikiwa kwa haraka naye kushiriki. Angehakikisha ambulance zinatoka na kwenda kusubiria wagonjwa.

Anakuja hapa anazunguka zunguka wakipiga stories na Chalamila.

View attachment 3153628
Ndivyo mambo nchi hii yalivyo.
Umesahau kule bukoba ya precision helcopter ya kumwaisha waziri mkuu ilikuwepo huku ya kuwapeleka waokoaji na vifaa ikichelewa, halafu huyu huyu chalamila na waziri mkuu wako hapo wapiga maneno kwa waandishi wa habari wakiwa wamefunikwa na miamvuli.
Kuna muda unawaza sisi huwa tunafikiri kwa namna gani. Ndicho hiki hiki kitakachotokea hapo.
 
Back
Top Bottom