Chalamila anatafuta umaarufu hata kwa mambo yasiyo na maana wala ulazima.
Hivi kuna mahali imendikwa wakristo wazikwe kwa bajeti fulani?
Tangu kale maziko yalifanyika kwa namna familia inavyoamua.
Bwana Mwokozi wetu alizikwa kwenye kaburi lililoandaliwa na Joseph wa Arimataya, kaburi la kuchongwa ndani ya mwamba, lenye mlango, kaburi alilokuwa ameliandaa kwaajili yake na wanafamilia wake. Hili kwa nyakati hizo lilikuwa ni kaburi la gharama kubwa.
Lakini walikuwepo waliokuwa wakizikwa kwenye makaburi yale ya kuchimba ndani ya saa 1 limekamilika.
Kwa hiyo, vyovyote wanafamilia wanavyoamua ni sahihi, maadam hawamlazimishi mtu.
Kwa taratibu za Kikristo, haijalishi unazikwa kwenye kaburi la namna gani, unazikwa baada ya muda gani, unazikwa kwa bajeti gani, ibada ya maziko ni ile ile. Mambo mengine ni uhuru wa wanafamilia kwa namna ile inayowapa faraja wao.
Kama anapendezwa na taratibu za Kiislam, hatakiwi kusubiri mpaka afe, bali anatakiwa kuslimu kuanzia sasa ili awe na ujakika wa kulazwa kaburini kwa mwongozo wa dini ya kiislam.