Chalamila: Nilikuwa likizo kama Injini ya gari lililoharibika

Kama alikuwa likizo ni kitu gani alikuwa anafanya.Kama ana nafasi nzuri awekeze vijana wapate ajira. We unafikiri wale vijana alioenda kuwaonya kule shule wakimaliza wataenda wapi.
 
Sioni mwaka au mwaka na nusu huyu Chalamila akiendelea kuwa RC, a year or 2 years naona Mh. Rais akimtumbua tena and it will be for good..!! He is not a leader at all, full stop..!!
 
Hawezi kubadilika, watu wa hivi ndio inabaki hivi sijui ndio hulka, mie toka udogon mtu wa vituko, nikikutana na watutuliosoma pamoja tukiongea kidogo watacheka na kusema makaveli hubadiliki, mke wangu kaishaongea naona anaanza kuzoea, mama yangu nae kadhalika.

Kama ilivyo umbea, usengenyaji, uvivu, tupo na sisi watu wa vituko
 
Sioni mwaka au mwaka na nusu huyu Chalamila akiendelea kuwa RC, a year or 2 years naona Mh. Rais akimtumbua tena and it will be for good..!! He is not a leader at all, full stop..!!
Acheni kumchulia,kwani Kazi hapigi? Kwa nini umhukumu kwa mambo yasiyo na tija?
 
Mnaopenda maisha ya kinafiki ndo mnamuona sio kiongozi! Chalamila is real not feck kama walivyo viongozi wengi!
Chalamila sio mnafiki kama wewe ujue,Kazi anaiweza Sana tuu ila hulka yake iachwe maana Agrrey Mwanry na Makongolo Wako hivyo pia..

Chalamila aachwe apunguze umaskini huko Kagera.
 
Sioni mwaka au mwaka na nusu huyu Chalamila akiendelea kuwa RC, a year or 2 years naona Mh. Rais akimtumbua tena and it will be for good..!! He is not a leader at all, full stop..!!
Hao walioteuliwa kuchukua nafasi yake wameshindwa ndio maana karudiwa yeye tena
 
Habari Wana JF,

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila Amesema alikuwa likizo tuu kama Injini ya gari lililoharibika..

Kuharibika kwa Board haimaanishi Injini ni mbovu.👇

===

MKUU wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema alikuwa likizo kama injini ya gari lililoharibika.
Ameyasema hayo leo Agosti 4, 2022 wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge.

Amesema kwa sasa amerudi kama gari jipya na yuko tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, amewetaka Wakuu wa Wilaya mkoani humo kufanya kazi kwa bidii kwani vyeo vya kuteuliwa ni vya mzunguko na kila mmoja Mungu umpa kwa wakati wake.

Amesema kama watafanya kazi kwa hofu ya kutoteuliwa tena basi wataaribu kazi na kushindwa kuwatumikia wananchi.

Amesema utekelezaji ambao ataanza nao ni maagizo ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu,wakati alipofanya ziara yake mkoani Kagera na kuwataka viongozi kuhakikisha wanatafuta njia ya kuufanya mkoa wa Kagera kuwa mkoa mwenye uchumi wa juu kwa sababu unakila kigezo cha kuwa Mkoa wenye uchumi mkubwa.

Awali akikabidhi ofisi Jenerali Mbuge alimuomba mkuu huyo wa mkoa kufanikisha maswala ya kitaifa kwa kuanza na Sensa ya watu na makazi, kufanikisha kuhitimisha mbio za mwenge kitaifa, kuhakikisha mradi wa bomba la mafuta unafanikiwa na wananchi wanalipwa fidia.

Source: Habari Leo
Afisa kipen
 
Chalamila sio mnafiki kama wewe ujue,Kazi anaiweza Sana tuu ila hulka yake iachwe maana Agrrey Mwanry na Makongolo Wako hivyo pia..

Chalamila aachwe apunguze umaskini huko Kagera.
Hata hujaelewa nilichomaanisha! Nilimjibu jamaa kuwa Chalamila ndo alivyo sio mnafiki kama viongozi wengine!
 
Huyo karudi kundini,kuna sababu nyuma ya yeye kurudishwa.
 
Hata hujaelewa nilichomaanisha! Nilimjibu jamaa kuwa Chalamila ndo alivyo sio mnafiki kama viongozi wengine!
SAFI sana. Wapumbavu wananyukana wao kwa wao. Kujua kusoma ni jambo moja. Kuelewa ni biashara nyingine. Mpuuzi mwenzio hajakuelewa. Kama sio wapumbavu mtaelewa: You can't live crooked and think straight as you can't live straight and think crooked! Mti twaujua kwa matunda yake. Huyo bwana ni character. Kuna wakati alisema: katiba yetu ina matatizo. Kuna siku makamu wa rais atamroga rais ili achukue hiyo nafasi. Aliyasema hayo wakati mkuu wake amesema amekuwa mkuu kwa kudra za Mwenyezi Mungu na kwa mujibu wa katiba. Uchizi mtupu. Chawa wadudu wanachagua mahali pa kukaa. Lakini ninyi kwa Chalaboy mnakaa kihasara. Inasikitisha.
 
Chalamila mtoto wa fukara??? tuulize wanyalu tutakwambia...kwa taarifa yako Chalamila ni royal family...ukoo wa Chalamila una link ya damu na ukoo wa Mkwawa wana ukwasi tangu 1800s mwishoni...wanazijua bunduki, mavazi na pesa miaka mingi sana, huyo Chalamila unaemuona haujui umaskini...
Acha kuwa chawa wake basi.
Niambie Royal family gani hapa Tz mtoto wao ni mwalimu wa govt?
Kumbuka Chalamila alikuwa mwalimu.
 
Habari Wana JF,

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila Amesema alikuwa likizo tuu kama Injini ya gari lililoharibika..

Kuharibika kwa Board haimaanishi Injini ni mbovu.👇

===

MKUU wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema alikuwa likizo kama injini ya gari lililoharibika.
Ameyasema hayo leo Agosti 4, 2022 wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge.

Amesema kwa sasa amerudi kama gari jipya na yuko tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, amewetaka Wakuu wa Wilaya mkoani humo kufanya kazi kwa bidii kwani vyeo vya kuteuliwa ni vya mzunguko na kila mmoja Mungu umpa kwa wakati wake.

Amesema kama watafanya kazi kwa hofu ya kutoteuliwa tena basi wataaribu kazi na kushindwa kuwatumikia wananchi.

Amesema utekelezaji ambao ataanza nao ni maagizo ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu,wakati alipofanya ziara yake mkoani Kagera na kuwataka viongozi kuhakikisha wanatafuta njia ya kuufanya mkoa wa Kagera kuwa mkoa mwenye uchumi wa juu kwa sababu unakila kigezo cha kuwa Mkoa wenye uchumi mkubwa.

Awali akikabidhi ofisi Jenerali Mbuge alimuomba mkuu huyo wa mkoa kufanikisha maswala ya kitaifa kwa kuanza na Sensa ya watu na makazi, kufanikisha kuhitimisha mbio za mwenge kitaifa, kuhakikisha mradi wa bomba la mafuta unafanikiwa na wananchi wanalipwa fidia.

Source: Habari Leo
Kaanza tena kuzomoka😀
 
Acha urongo

Kina Chalamila wako wengi kama Sanga au Massawe

Huyu haitoki kwa Ramadan Chalamila mbia wa Kwacha enzi zile

Huyu ni kule Ugalatiani kwa akina Betty Mkwasa
Chalamila wote ni ukoo mmoja acha kuongopea watu
Acha kuwa chawa wake basi.
Niambie Royal family gani hapa Tz mtoto wao ni mwalimu wa govt?
Kumbuka Chalamila alikuwa mwalimu.
Kubishana na popoma sifanyi hiyo kazi. Amini unavyoamini. kwa heri.
 
Back
Top Bottom