Huyu mnyalukolo, volioja vya manebo ni asili yake. Hata wakati wa Magufuli, aliwahi kumshukuru na kumsifu Magufuli kwa kumletea mkurugenzi mrembo. Magufuli akang'aka kuwa aache tamaa.
Lakini Chalamila ni maneno tu, hata wakati ule, hatukuwahi kusikia, iwe kwa uwazi au kwa zile taarifa za chini chini kuwa aliwahi kuhusishwa na mambo yale machafu ya kuteka watu kama vijana wenzake waliokuwa kwenye nafasi yake, walikuwa wakifanya.
Mnyalu hana neno na mtu, na hata alipotenguliwa, hakuonekana kuchanganyikiwa, aliendelea kuonesha tabasamu la maisha ya furaha.
Mnyalu, usitikisike, fanya kazi kadiri uwezo unavyoruhusu, lakini usipoteze utu kwa kujipendekeza, wala usidhulumu uhai wa mtu kwaajili ya kulinda cheo. Makosa mengine yote yana msamahala, lakini mauaji na dhuluma hutengeneza laana. Mwangalie mwenzako alitekuwa mwamba wa Dar, na hakika lazima, ataandamwa na laana yeye na kizazi chake.