PostGE2025 Chalamila: Polepole alikuwa Balozi, mimi kama mkuu wa mkoa sijui alijiuzulu akiwa nchi gani

PostGE2025 Chalamila: Polepole alikuwa Balozi, mimi kama mkuu wa mkoa sijui alijiuzulu akiwa nchi gani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila amewataka wananchi waendelee kuliamini na kuliacha Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi wa kutokewa kwa aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole.

Chalamila amesema hayo leo Ijumaa, Desemba 5, 2025 wakati akijibu swali aliloulizwa kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Swali hilo limetaka kujua kama Chalamila amewahi kwenda kumtembelea mama yake Polepole na au Polepole mwenyewe yupo wapi kwani alitoweka akiwa mkoani mwake.

Oktoba 6, 2025, taarifa zilisambaa mitandaoni zikidai Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM) ametekwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na mpaka sasa hakuna taarifa zozote juu yake.

Akijibu swali hilo, Chalamila amesema matatizo katika mkoa huo yapo mengi na hawezi kwenda kumtembelea kila mmoja na huo hautakuwa uongozi.
"Polepole alikuwa Balozi, mimi kama mkuu wa mkoa sijui alijiuzulu akiwa nchi gani," amesema na akisisitiza hakuna utaratibu wa Balozi anapokuja nchini kwenda kuripoti kwa mkuu wa mkoa.

Amesema alisikia tu kwamba amechukuliwa:"Kumbe alikuwa Dar es Salaam...Sina taarifa zozote ninazoweza kumzungumzia (Polepole) zaidi nilikuwa naangalia YouTube tu yale anayoyasema kwani hayakuonyesha alikuwa anazungumzia akiwa wapi."

Chalamila amesema majibu yaliyotolewa na Polisi:"Tuwape muda waendelee na uchunguzi, kama nilivyosema upelelezi unategemea na aina ya tukio."
1764940521861.png

Chanzo: Mwananchi
 
Akizungumza leo Desemba 5, 2025 katika Hafla ya Uzinduzi wa Mita Janja za Umeme kwa Wateja wa TANESCO katika Ukumbi wa JNICC, RC Chalamila amesema kuhusiana na taarifa za alipo Balozi Humphrey Polepole yeye binafsi hajui akieleza suala hilo lipo mikononi mwajeshi la polisi waachiwe wafanye uchunguzi

 
Muda mfupi uliopita hapo hapo alitamka kuwa ni jukumu lake kama mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha usalama kwa raia wote Dae es salaam, Kaulizwa kuhusu mkazi wa Dar es salaam Polepole, anajibu hafahamu 😀 hii ni zaidi ya comedy
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila amewataka wananchi waendelee kuliamini na kuliacha Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi wa kutokewa kwa aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole.

Chalamila amesema hayo leo Ijumaa, Desemba 5, 2025 wakati akijibu swali aliloulizwa kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Swali hilo limetaka kujua kama Chalamila amewahi kwenda kumtembelea mama yake Polepole na au Polepole mwenyewe yupo wapi kwani alitoweka akiwa mkoani mwake.

Oktoba 6, 2025, taarifa zilisambaa mitandaoni zikidai Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM) ametekwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na mpaka sasa hakuna taarifa zozote juu yake.

Akijibu swali hilo, Chalamila amesema matatizo katika mkoa huo yapo mengi na hawezi kwenda kumtembelea kila mmoja na huo hautakuwa uongozi.
"Polepole alikuwa Balozi, mimi kama mkuu wa mkoa sijui alijiuzulu akiwa nchi gani," amesema na akisisitiza hakuna utaratibu wa Balozi anapokuja nchini kwenda kuripoti kwa mkuu wa mkoa.

Amesema alisikia tu kwamba amechukuliwa:"Kumbe alikuwa Dar es Salaam...Sina taarifa zozote ninazoweza kumzungumzia (Polepole) zaidi nilikuwa naangalia YouTube tu yale anayoyasema kwani hayakuonyesha alikuwa anazungumzia akiwa wapi."

Chalamila amesema majibu yaliyotolewa na Polisi:"Tuwape muda waendelee na uchunguzi, kama nilivyosema upelelezi unategemea na aina ya tukio."
View attachment 3511600
Chanzo: Mwananchi
KAMA NI SIMU TUNA SEMA IPO KWENYE AEROPLANE MODE
 
Desemba 17, 2025
RC CHALAMILA ATAKA TCTA UKONGA KUZINGATIA UTAFITI ZAIDI -

View: https://m.youtube.com/watch?v=L-el4tmZ8TI

Anawasihi wahitimu wa Chuo cha Urekebishaji cha Tanzania Ukonga jijini Dar es Salaam kutumia maarifa na ujuzi walioupata katika kazi zao kama maafisa wa magereza.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amesema haya leo, Desemba 17, 2025, wakati wa mahafali ya tatu ya Stashahada ya Kozi ya Sayansi ya Urekebishaji katika Chuo cha Urekebishaji cha Tanzania Ukonga jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila, akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alipongeza juhudi zinazofanywa na chuo hicho katika kutoa elimu bora, akikihimiza chuo hicho kuendelea kufanya maboresho mbalimbali ili kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

Pia alielezea umuhimu wa chuo hicho kuzingatia utafiti utakaosaidia kukuza chuo hicho. Zaidi ya hayo, RC Chalamila ametoa Stashahada kwa wanafunzi 44 ambao wamekidhi mahitaji ya sheria na kanuni za Chuo cha Sayansi ya Urekebishaji cha Tanzania na wanastahili kupewa Stashahada ya Sayansi ya Urekebishaji.

Sambamba na hilo, RC Chalamila amemkabidhi zawadi mwanafunzi mmoja, Bi. Idda P. Danda, ambaye alifanya vizuri zaidi kitaaluma miongoni mwa wanafunzi 44 aliowatunuku Stashahada ya Sayansi ya Marekebisho. Hatimaye, kabla ya kuhitimisha sherehe ya tatu ya mahafali ya chuo hicho, RC Chalamila amepokea ombi la taa za jua kutoka kwa Mkuu wa chuo ili ziweze kuwekwa katika maeneo mbalimbali ya chuo ambapo amewaomba wamletee ofisini kwake uchambuzi wa mahitaji ya taa hizo ili ofisi yake iweze kuona jinsi ya kusaidia.
 
Back
Top Bottom