DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila amewataka watanzania kuwa na imani na Jeshi la Polisi katika kipindi hiki wakifanya uchunguzi juu ya waliotekeleza shambulizi dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima.
Akizungumza na vyombo vya habari leo May 02, Jijini Dar Es Salaam Chalamila amesema “wako walio na mashaka juu ya statement ambayo imetolewa na Jeshi la Polisi nawaomba waendelee kuwa na usikivu mkubwa sana na kwa wale ambao wameonyesha mashaka kwa Jeshi la Polisi wawe na imani kubwa ana kwamba vyombo vya dola havitamuonea yeyote”
Chalamila ameongeza pia kwa wale ambao watabainika kuhusika katika tukio hili watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vinavyohusika.
“waliohusika watafikishwa kwenye vyombo husika na hatua kuchukuliwa aliyefanya jambo hili atabainika” ameongeza Chalamila.
Pamoja na hayo ametoa wito kwa watanzania kuachana na dhana ambayo inaenezwa ikiihusisha serikali pamoja na masuala ya kisiasa katika kudhuriwa kwa Padre Kitima.
“wanabainisha kuhusisha jambo hili na mambo ya serikali au na mambo ya kisiasa na kuonyesha kwamba serikali imehusika sioni mantiki ya serikali ama siasa kufurahia jambo hili” amesema Chalamila
Aidha Chalamila amelaani vikali tukio hilo ambalo limemgusa yeye kama kiongozi wa serikali, mtu aliyewahi kufanya chini ya Padri Kitima pamoja na muumini wa kanisa Katoliki.