Chalamila: Suala la Padri Kitima litakuwa na uwazi lakini kwa kufuata miiko ya taaluma

Chalamila: Suala la Padri Kitima litakuwa na uwazi lakini kwa kufuata miiko ya taaluma

Bora kumuamini Shetani kuliko kuliamini Jeshi la polis Tz
 
Mhh sisi maduwanzi si ndivyo?

Serikali ijifunze kuja na ushahudi acheni kutuma maduwanzi wasio na hoja kujibu vitu vya msingi.
Ukweli ni kwamba matukio yote yasiyoeleweka Watanzania wote tunayaona na hakuna moja lililojibiwa kwa ushahidi wa msingi.
Inakuja haitowezekana Tena kupumbaza mtu sababu mnajaza sumu Kali Sana kwenye mioyo ya watu wasio na ubaya Watanzania raia wema kabisa waaminifu
 
Mkumbusheni Chalamila anapokaa kwenye vikao vya vya ulinzi na usalama wa mkoa. Hili bado halijaisha.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila Albert Chalamila amewataka Watanzania kuwa na imani na Jeshi la Polisi katika kipindi hiki wakifanya uchunguzi juu ya waliotekeleza shambulizi dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima.

Akizungumza na vyombo vya habari leo May 02, Jijini Dar Es Salaam Chalamila amesema “wako walio na mashaka juu ya statement ambayo imetolewa na Jeshi la Polisi nawaomba waendelee kuwa na usikivu mkubwa sana na kwa wale ambao wameonyesha mashaka kwa Jeshi la Polisi wawe na imani kubwa ana kwamba vyombo vya dola havitamuonea yeyote”

Chalamila pia amesema kwa wale ambao watabainika kuhusika katika tukio hili watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vinavyohusika.

“waliohusika watafikishwa kwenye vyombo husika na hatua kuchukuliwa aliyefanya jambo hili atabainika” ameongeza Chalamila.

Pia soma
  1. Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
  2. Rais wa TEC, Askofu Pisa apingana na polisi, asema taarifa yao kuwa Padri Kitima alikuwa anapata kinywaji wakati anashambuliwa ni Upotoshaji

Pamoja na hayo ametoa wito kwa watanzania kuachana na dhana ambayo inaenezwa ikiihusisha serikali pamoja na masuala ya kisiasa katika kudhuriwa kwa Padre Kitima.

“wanabainisha kuhusisha jambo hili na mambo ya serikali au na mambo ya kisiasa na kuonyesha kwamba serikali imehusika sioni mantiki ya serikali ama siasa kufurahia jambo hili” amesema Chalamila

Aidha Chalamila amelaani vikali tukio hilo ambalo limemgusa yeye kama kiongozi wa serikali, mtu aliyewahi kufanya chini ya Padri Kitima pamoja na muumini wa kanisa Katoliki.


View attachment 3322738
Wala hatutaki kuwajua maana sie tumesha muachia Mungu. Tuna subiri adhabu ya Mungu.
Sisi Wakristo huwa hatulipi visasi maana Mungu alisha tauhidi visasi ni vyake. Kuweni na amani
 
Back
Top Bottom