Chalamila: Wakubwa wa madawa ya kulevya tumewakamata, hatuwataji

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Akiongea asubuhi hii kupitia television ya ITV mkuu wa mkoa wa dar es salaam ndugu Albert chalamila amesema kuwa wamewakamata wakuu kabisa wa madawa ya kulevya aina ya heroin baada ya kukamata tani tatu za madawa hayo yenye thamani ya zaidi ya billion 100 ila hawatawataja kwa sasa kwakuwa kuwataja kutaharibu upelelezi.[emoji23]

Kawaida mi nilijua kuwa ukimkamata muuzaji mdogo au wa kati wa madawa ya kulevya humtaji ili usiharibu upelelezi ili umkamate bosi wake.

Sasa umeshamkamata big boss wa madawa ya kulevya unaogopa kumtaja kwa kuogopa kuharibu upelelezi upi? Au unataka uwakamate wale wadogo?

Si umeshamkamata bosi huyu si ndo anawajua wadogo wote?

Sema 100 billion ni hela nyingi sana ngoja tuone iyo haki inavyofanya kazi.[emoji23][emoji23] Mae


Pia soma: Kutotaja jina la papa wa madawa ya kulevya ni kutengeneza mazingira ya ufisadi
 
Siasa za matukio
 
Itakua CCM yenyewe ndo kinara wa kuuza madawa ya kulevya,
 
Utakuja kuambiwa utaratibu wa kukamata na kusachi haukufuatwa kwa hiyo Jaji ametupilia mbali kesi.
 
Wao waseme tu hao ni vijana wa kawaida tu wasio na majina mjini na wameweza kuwakamata baada ya wenyewe kudhulumiana au kushindwa kukubaliana kimaslahi na wale jamaa zetu.
 


Ni kwamba upeo wako mdogo na akili huna, unafikiri hayo Madawa yanalimwa Tanzania? Hao vigogo wana connection duniani.
 
Movie tu hiyo hata mahakamani hawatafikishwa kuepuka kuharibu upelelezi.

Kukamata siku hiyohiyo na kujua aina,uzito na bei ya soko ila upelelezi kukamilika miaka kumi.

Na ukikamilika mtaambiwa ni unga wa ngano siyo heroin tena.
 
Ni kwamba upeo wako mdogo na akili huna, unafikiri hayo Madawa yanalimwa Tanzania? Hao vigogo wana connection duniani.
Mimi huwa siangaliagi narcos bana wewe pekeyako ndo unawajua kina Escobar, El. Chapo, black widow....
 
Hao jamaa hawatakaa wasikike tena, na wala hatutakuja kujua wapi hii kesi yao iliishia, ndio maana Chalamila ameamua kuturusha roho tumuone yupo kazini kumbe kwa upande mwingine anatuletea michezo tu ya kisiasa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hayo ndo yanayoongoza uchumi wa nchi..
 
Nalo litapita kama lile la jezi fake. Yani hadi waziri alikiwa na kigugumizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…