Chalamila: Wakubwa wa madawa ya kulevya tumewakamata, hatuwataji

Waachie wataalam acha kujifanya kila kitu.
 
Muongo tu huyo. Eti hatuwataji nani kakuuliza uwataje, stupid RC
Unapomkamata boss lazima uendeleze utaratibu wa kukamata visaidizi vyote vyote roots, zote aider wote bila kuharibu upelelezi / kwa ukubwa huu wa mzigo, vigogo wa serekalini hawakosekani, tuache uropo uropo na upopoma wa kihayawani.
 
Mh kanifurahisha....sasa kulikuwa hakuna haja hata ya kutueleza, walimalize kimya kimya tu. Mtaani tutaona mateja wanapungua hivi karibuni!
 
Niko nae kwenye foleni
 

Attachments

  • IMG_20231206_173733_449.jpg
    1.8 MB · Views: 4
Akikamatwa mpika gongo anaoneshwa kabisa runingani pamoja na mitambo yake! Ahahahahaha!!!
 
Drugs kingpin mkuu ni Kin. Kin. Ngmbl Mwr

Wamemkamata????
 
Ndugu Mkuu wa Mkoa, Hivi hili sakata liliishia wapi? 😛 😛 😛 Hawa wahalifu walikamatwa? je walifikishwa mahakamani kujitu mashtaka haya ya wizi na uhujumu uchumi.


View: https://youtu.be/e74-ozak_Gs
 
Huyu msanii walimleta dar ili awasaidie uigizaji. Makonda aliwataja na hadharani wauza madawa bila woga ikaleta matokeo mazuri sana. Sasa tangu mama kaingia kawaruhusu wauza madawa kwa kuwapa ishara ya taa kijani. Wameshafungua soko sasa wanajua uchaguzi karibu wanatuletea maonyesho. Huenda hata hayo madawa ukakuta ni unga wa sembe yote. Vinginevyo hapo utafanyika uhuni watapiga hela ya kuhongwa mzigo utatoka.
 
Hivi wanahabari wetu wameshindwa kunusa chochote kile juu ya hili sakata ama wahusika wake!?. JF ni jukwaa kubwa, kama wahusika wadogo kwenye jinai majina yao huwa yanawekwa hadharani, hii "double standard" inatokea wapi!?

Kama kuna majina ya vigogo serikalini ama bungeni ni vyema yakaanikwa. Mzigo wa bwimbi wenye thamani ya TZS 100Bn si mchezo wa kitoto hata kidogo. Kuna mzito mmoja pale bungeni na mtoto wa namba.... hapa nchini sijui kama wataikwepa kashfa hii
 
Kazabuti Chalamila wapo wengi sana hao, ni mitandao mingi ambayo haiingiliani.
 
Ujanjaujanja Tu Mwakani Uchaguzi Serikali Ya Mtaa
 
Kama hawawezi kuwataja wamwite afande mroto awasaidie, tena yeye atawaonyesha kwenye TV na kuwapigapiga kwenye mabega........watapata tabu sana, kipigo chake ni cha mbwa koko😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…