Chalamila: Wakubwa wa madawa ya kulevya tumewakamata, hatuwataji

Ooh
 
Hatari sana,

Chalamira hana uwezo wa kukamata Drugs Kingpins awamu hii.. sidhani hata kile kiti kule juu nacho kinaweza kuwakamata au hata kutoa amri dhidi yao.

Sio kazi yake, vipo vyombo vyenye kazi hiyo
 
kiherehere....si angepiga kimya mpaka wakate chain yote
 
Movie tu hiyo hata mahakamani hawatafikishwa kuepuka kuharibu upelelezi.

Kukamata siku hiyohiyo na kujua aina,uzito na bei ya soko ila upelelezi kukamilika miaka kumi.

Na ukikamilika mtaambiwa ni unga wa ngano siyo heroin tena.

..Je, ni sahihi kutaja " thamani " ya madawa yaliyokamatwa?

..kama utaratibu baada ya kukamata madawa ni kuyaharibu na si kuyauza kwanini tunajishughulisha kujua thamani yake?
 
Saf sana, bora asiwatqje, kipindi cha JPM aliwataja mkapiga sana kelele eti anaharibu brand za watu. Nyie mazuzu hamjulikani mnataka nini
 
Halafu huwa najiuliza sana swali hili,

Kama na wao sio wauzaji wa madawa ya kulevya wanawezaje kujuwa thamani ya mzigo ..?

Hiii biashara Ina mkono mrefu sana aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…