Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Watu wanataka bure tu kila kitu!
Yani hata wakipeana mimba kwa starehe zao wanataka serikali iwahudumie bure!

Hii serikali nayo ndio imewazoesha mambo ya burebure ili Kupata sifa za kijinga.

Weka gharama reasonable lakini bure ni uamuzi usio Sahihi.

Kama hiyo elfu 40 iko reasonable
Haya, elimu nayo waweke Ada kila mtoto atoe Ada elfu 20 iende serikali kuu.
Waalimu Wapate mishahara, marupurupu na serikali isipate Mzigo kuchukua pesa kwenye sekta zingine

Kila sekta ijihakikishie inajitegemea kwa angalau asilimia 50
 
Robert Heriel Mtibeli
Huenda haujui Umasikini au umekuzwa katika mfumo wa mafanikio acha nikae kimya.

Mkuu Mim nimekua kwenye jamii Maskini, nimezaliwa huko, nimesoma huko.

Pamoja na Umaskini WA nyumbani kwetu lakini walionilea miaka yote waliamini katika falsafa ya lazima nichangie chochote popote pale nilipo. Bure! Bure ni matusi. Bure ni kujidhalilisha, bure sio UTU.

Nimekuzwa hivyo na katika mazingira ya umaskini.
 
Shida watanzania wengi hawajui kitu kinaitwa savings yaani kuweka akiba ya pesa yako. Mfano mzuri watu wengi wanalalamika January ni ngumu ukiuliza sababu watakwambia ada ina maana kuanzia mwezi wa kumi hawakujua kama wanatakiwa walipe ada January? Laiti wangekuwa wanasave pesa zao kila mwezi pengine wangelipa ada kiurahisi na kukabiliana na matatizo madogomadogo.
 
Shida watanzania wengi hawajui kitu kinaitwa savings yaani kuweka akiba ya pesa yako. Mfano mzuri watu wengi wanalalamika January ni ngumu ukiuliza sababu watakwambia ada ina maana kuanzia mwezi wa kumi hawakujua kama wanatakiwa walipe ada January? Laiti wangekuwa wanasave pesa zao kila mwezi pengine wangelipa ada kiurahisi na kukabiliana na matatizo madogomadogo.

Tanzania bado tunasumbuliwa na ujamaa akilini.
Tunajua ikifika January tutalialia kwa ndugu au kwa Mkuu WA shule
 
Back
Top Bottom