Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Mkuu una uhakika nchi yetu maskini? Sidhani kama ni maskini. Binafsi nadhani ni usimamizi wetu hafifu au mbovu katika kusimamia rasilimali zetu hasa za asili [madini, gasi,mazao n.k ] na hivyo kushindwa linda au jenga uchumi wa mwananchi wa kawaida.

Embu jiulize uchumi wa wa Tanzania umehodhiwa na kina nani kwa asilimia kubwa? Anzia visiwani mpaka upande wa bara, utaniambia.

Jambo lingine ni vipaumbele. Hatujaweka vipaumbele baadhi ya mambo au tumeweka lakini hatutimilizi hivi vipaumbele, ndo maana utaenda taasisi ya serikari utakosa huduma sababu, hela haijapelekwa.

Hivi mbona hela za kufanya issues ambazo mwananchi wa kawaida hafaidiki nazo mbona zinapatikana na wanaozifuja hwajali wala kuwaonea huruma hawa wanaohangaika zaidi ya kutaka wawachague?
 
Hivi ninani aliye wahi kupata huduma bure!
Kinacho lalamikiwa ni mawasilisho ya hoja na si hoja.

Mkuu ukienda hospital watu wanalia Sana. Gharama za Upasuaji serikali kwenye Mimba na kujifungua sio chini ya 150k Mpaka unatoka sio ajabu ukatoa 200k

Watu wengi wanalia wakati wangekuwa na Bima ingekuwa elfu 40 tuu
 
Mkuu una uhakika nchi yetu maskini? Binafsi nadhani ni usimamiI wetu hafifu au mbovu katika kusimamia rasilimali zetu hasa za asili [madini, gasi,mazao n.k ] na hivyo kushindwa linda au jenga uchumi wa mwananchi wa kawaida. Embu jiulize uchumi wa wa Tanzania umehodhiwa na kina nani kwa asilimia kubwa? Anzia visiwani mpaka upande wa bara, utaniambia. Jambo lingine ni vipaumbele. Hivi mbona hela za kufanya issues ambazo mwananchi wa kawaida hafaidiki nazo mbona zinapatikana na wanaozifuja hwajali wala kuwaonei huruma hawa wanaohangaika zaidi ya kutaka wawachague?

Umaskini unaanzia kwenye mindset na mentality.
Kisha ukishakuwa na mentality ya kimaskini hata usimamizi unakuwa ni mbovu hata kama kuna rasilimali za kuwafanya watu wawe na fedha.

Moja ya mindset ya Mtu Maskini ni kupenda burebure
 
Ukikata hiyo bima unaitumia hapo hapo au unachangia kwa muda wa miaka miwili kwanza?
Hebu weka hapa hivyo vigezo vya hiyo bima ya elfu 40 halafu tuone mtu akipata ujauzito ndani ya miezi 9 kama ita cover huduma za kujifungua.

Ukikata hiyo ya 40, ndani ya wiki mbili inafanya Kazi.

Hivyo kama Mwanamke atagundua ni mjamzito ule mwezi wa Kwanza anaweza kukata kisha first trimester anaanza Kliniki Akiwa na Bima. Anakula Raha za Mimba bila stress za kuwaza itakuwaje
 
Serikali isikwepe jukumu lake.

Jamani tembeeni muone, kuna watu wana maisha magumu ukimwambia aitoe 40 kwa pamoja ni bora umpige kisu, HANA, kuna watu wana maisha magumu huko.

Mfano mzuri kuna ile video yule mzee anatembea na samaki akapewa 20k mpaka akatoa machozi ya shukrani, vijijini huko kuna wakina mama wanalipa vipande ama mraba 20 kwa 20 ama 10 kwa 10, hizo ni mita kwa elfu saba.

Anaweza kumaliza siku 2 mpaka 3, sasa jiulize kazi ya elfu 7 amalize kwa siku 3 ama 2, kwa siku kaingiza kiasi gani, anakula kiasi gani, bajeti ya hospital kiasi gani, shule mtoto kiasi gani, umeme ama solar, ama mafuta ya taa, ama miahumaa kiasi gani, na hizo kazi ni za msimu

Serikali itoe hudumu muhimu ikiwezekana bure, elimu bure, afya bure inawezekana kabisa.. Mkuu wa wilaya, sijui nani nani wanatembelea gari za milioni 400 huko, je pesa hizo hazitoshi kuhudumia afya na elimu wilaya husika!?

Na huduma hizo zisiwe bure tu ila ziwe ni bora kabisa.
 
Aisee hili taifa ni kutafuta hela halafu kaa kimya watu akili bado hazijawakaa!, unazungumzia bima nawakati hospitali haina vifaa..??! mbona vitu viwili tofauti nawakati wenye bima tu ya mapesa kushinda hiyo wanapataga kasheshe haya huyo wa 40,000!. watanzania baadhi kuna nati zimelega mahali!.
 
Alafu hiyo Bima Sisi wengine wabangaizaji tunaitumia kama dharura hasa tukiona NHIF inatuletea mushkeli. Yaani kipato kinazingua
Wazeee wetu waliokua na uchumi average sana mama akiwa mjamzito wanakua na maandalizi mengi sana kuanzia fedha, usafiri, vyakula siku za awali za uzazi( ndizi, nyama mara nyingi wanachinja kuku kadhaaa baadae mbuzi) na wamama nao wanakua washajua ataenda na nani hospital na nani atamhudumia akishajifunguua
 
Serikali isikwepe jukumu lake.

Jamani tembeeni muone, kuna watu wana maisha magumu ukimwambia aitoe 40 kwa pamoja ni bora umpige kisu, HANA, kuna watu wana maisha magumu huko.

Serikali itoe hudumu muhimu ikiwezekana bure, elimu bure, afya bure inawezekana kabisa.. Mkuu wa wilaya, sijui nani nani wanatembelea gari za milioni 400 huko, je pesa hizo hazitoshi kuhudumia afya na elimu wilaya husika!?

Na huduma hizo zisiwe bure tu ila ziwe ni bora kabisa.

Mkuu ndio maana serikali imeweka elfu 40.
Hiyo gharama ni reasonable kwa Tanzania yetu lakini kuiondoa iwe bure Kabisa huo utakuwa Wehu.

Unajua kulima kibarua heka Moja Kwa sasa kijijini ni elfu 30-40

Mtu kuwa Maskini haimaanishi asiwajibike.

Kutowajibika kunaondoa UTU wa binadamu.

Na Sisi Watibeli Moja ya mambo tunayoyalinda ni Hilo la UTU. Kuwajibika, kufanya kazi, ili kuchangia, kuonyesha mchango wako kwenye jamii inayokuzunguka
 
Aisee hili taifa ni kutafuta hela halafu kaa kimya watu akili bado hazijawakaa!, unazungumzia bima nawakati hospitali haina vifaa..??! mbona vitu viwili tofauti nawakati wenye bima tu ya mapesa kushinda hiyo wanapataga kasheshe haya huyo wa 40,000!. watanzania baadhi kuna nati zimelega mahali!.

Hivi mnataka vitu vya bure alafu mtegemee vifaa hospitalini, logically imekaa Sawa hiyo.

Watanzania wangapi wanalipa Kodi? Au Ndio ninyi mnasema tukinunua vitu ndio tunalipa Kodi?

Watu watoe Kodi wapewe huduma.

Mbona hela za pombe zinapatikana?
 
Back
Top Bottom