Serikali isikwepe jukumu lake.
Jamani tembeeni muone, kuna watu wana maisha magumu ukimwambia aitoe 40 kwa pamoja ni bora umpige kisu, HANA, kuna watu wana maisha magumu huko.
Mfano mzuri kuna ile video yule mzee anatembea na samaki akapewa 20k mpaka akatoa machozi ya shukrani, vijijini huko kuna wakina mama wanalipa vipande ama mraba 20 kwa 20 ama 10 kwa 10, hizo ni mita kwa elfu saba. Anaweza kumaliza siku 2 mpaka 3, sasa jiulize kazi ya elfu 7 amalize kwa siku 3 ama 2, kwa siku kaingiza kiasi gani, anakula kiasi gani, bajeti ya hospital kiasi gani, shule mtoto kiasi gani, umeme ama solar, ama mafuta ya taa, ama miahumaa kiasi gani, na hizo kazi ni za msimu
Serikali itoe hudumu muhimu ikiwezekana bure, elimu bure, afya bure inawezekana kabisa.. Mkuu wa wilaya, sijui nani nani wanatembelea gari za milioni 400 huko, je pesa hizo hazitoshi kuhudumia afya na elimu wilaya husika!?
Na huduma hizo zisiwe bure tu ila ziwe ni bora kabisa.