Kuna huduma ukienda na hako kabima kako hupati ng'o ni kabima kasicho na thamani hospitalini ni kabima ka kupata get pass ya kumuona daktari na kuandikiwa dawa za bei rahisi mno na kukiwa na vipimo vikubwa utaambiwa ulipie tu maana bima yako hairuhusu wewe kupata hio huduma dawa za bei juu huwezi kupata kwa hio bima mfano dawa za kuanzia 100,000/= na kuendelea hupati kwa hio bima lazima uambiwe ulipie tu
Ndio maana nikaorodhesha utanufaika na nini kwenye hiyo Bima.
Ultrasound bila Bima serikali ni Tsh 15,000 - 25,000 kutegemeana na hospital.
Lakini ukiwa na Bima ya Tsh 40k hutoi Pesa.
Kujifungua kwa OP serikali ni Tsh 150,000 - 300,000 serikalini ukiwa huna bima.
Ila ukiwa na Bima ya 40k hutoi Pesa yoyote.
Kulala usiku Mmoja kwenye vitanda vya hospital za serikali ukiwa huna bima, Tsh 10,000 to 20,000. Lakini ukiwa na Bima ya 40k hutoi hata Buku.
Hiyo Bima ya 40k ni ya watu wa kipato cha chini Sana ili nao Wapate matibabu.
Imesaidia wengi.
Hiyo Bima ya 40k
Unapima Magonjwa yafuatayo;
UTI
Malaria
Taifodi
Na Magonjwa yote ya bacteria.
Kama haitoshi, unaweza kucheki full blood picture
Sasa wewe unataka nini zaidi?
Magonjwa makubwa hata hizo Bima za Milioni Moja hayatibu.