Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 9,818
- 14,585
Kitu kinachokera na kufanya nisipende kutumia stendi za mabasi za umma kama Magufuli Terminal, ni mpangilio mbovu na vurugu. Serikali imetumia mabilioni ya pesa kujenga stendi zenye miundominu ya kisasa na muonekano wa kimataifa lakini siasa za kijinga zinafanya hizo stendi ziwe kama magulio ya mifugo.
Tunapokwenda stendi, mtu unahitaji utulivu, usalama na starehe kuanzia unapofika stendi mpaka kwenye safari yako. Kwa mtu uliyesafiri nchi nyingine zenye miundombinu kama ya Magufuli terminal unaweza kuelewa ninachosema. Inakuaje ndani ya stendi kuwe kama sokoni, kama mmeamua kuwe na wamachinga basi wangekaa nje kwa ajili ya usalama wa wasafiri, mali za wafanyabiashara na miundombinu ya stendi. Unafika stendi unaanza kusumbuliwa na wapiga debe, msongamano wa wamachinga na wazururaji. Yaani ni vurugu. Kwa nini kila eneo la umma liwe soko? Basi pekekeni wamachinga airport pia.
Tunaenda kwenye stendi binafsi za mabasi sio tu sababu ni karibu, lakini pia ustaarabu. Hawa wafanyabiashara wanajali usalama na utulivu wa wateja wao. Unaweza kuacha begi lako bila wasiwasi na kwenda chooni, huwezi kuthubutu pale Magufuli terminal.
Hakuna wapiga debe wala wazururaji kwenye stendi binafsi. Serikali itengeneze mazingira mazuri kabla ya kuvutana na wafanyabiashara. Mfanyabiashara kipaumbele chake ni kutoa huduma bora ili kuvutia wateja zaidi. Kama mazingira ya Serikali yanakwaza mipango ya mfanyabiashara, anakosa namna zaidi ya kutafuta njia mbadala.