BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kupitia kwa Wakili wa Chalinze Cement Company Limited, Melchisedeck Lutema ambaye pia ni Wakili wa Chama cha Kutetea na Kusemea Walaji Tanzania amesema kuwa Chalinze ni Kampuni ambayo ilisajiliwa Mwaka 2021.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Mei 8, 2023 Jijini Dar es Salaam amesema:
“Chalinze ilisajiliwa ili iweze kuzalisha cement, Sheria inasema mtu yeyote ambaye anaweza kona maslahi yake yataingiliwa ana uhuru wa kulalamika, na siyo lazima uwe na kiwanda cha cement au mashine za uzalishaji.”
Ameongeza kwa kusema: “Chalinze sio tapeli, na Chama cha Walaji sio matapeli, ni taasisi ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria na kwa kufuata taratibu zote za Sheria, sio wafanyafujo na walikidhi vigezo vya sheria.”
“Imejengeka picha kuwa hivi vyombo ni vya kutapeli, havipo n ani wasumbufu ambao lengo lao ni kuharibu uwekezaji, siyo kweli na umma unatakiwa kufahamu hilo.”
Aidha, Bernard Elia Kihiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kutetea na Kusemea Walaji Tanzania amesema chama hicho kilichoundwa Mwaka 2007 kupitia Sheria ya Makampuni Brela, ilipofika kabla ya mabadiliko ya Mwaka 2019 baada ya Sheria kuelekea kubadili na kuwa chini ya Ustawi wa Jamii, amefafanua kuwa wao pia wana lengo la kutetea haki za walaji.
Kihiyo amesema: “Tumekuwa sehemu ya kuchangia na kusemea walaji katika ngazi zote za juu na chini, mfano Mwaka 2003 tulienda Mahakamani na kuzuia Sim card ambayo ilikuwa inataka kuuzwa Tsh. 1,000, mambo yalienda mbele na kutaka na win win situation.
“Kwa sasa baada ya kuona kuna changamoto inayoweza kutokea katika biashara, ikatufanya tuone mtu mwenye nguvu kubwa sokoni anaweza kufanya lolote na kuathiri soko.
“Kinachotokea katika kazi zetu za kila siku ni kuwa tunaangalia katika jicho la mbali, inaweza isitokee leo au kesho.”