JF ni sehemu ya kipekee ambayo kama mtu hujui hatari za mtandaoni ni rahisi kujikuta sehemu usiyoitegemea.Humu kuna wanaopiga wake zao kila siku lkn wakiwa hapa watalaani wanaume wanaopiga wake zao,kuna waliooa na wanawatoto lkn siku zote wakiwa hapa watapozi kama single men,humu kuna mashoga na wasagaji lkn wakiwa hapa watalaani hivyo vitendo,humu kuna wavivu wasipenda kujishughulisha wanaringia mali za kaka lkn wakiwa humu posts zao ni zaweza kuwa za maana kiasi ukadhani ni watu wa maana kama vitu wanavyoviandika,kuna wengine tunajifanya tumeokoka kumbe tunatype huku mkono mmoja umeshika red wine.Pia hapa JF kuna tuna utamaduni wetu fulani wa kumjua na kumpicture mtu kutokana na posts zake,kama anaonekana wa maana kutokana na vitu vya maana anavyoandika na hii inawafanya wengi tujisahau na kujikuta tunawaamini kiasi cha kuwaleta hawa watu katika maisha yetu ya kweli,mwisho wake ndo hivi vilio.JF siku zote itabaki kuwa salama kwa wenye kujua nini hatari za kwenye mitandao na siku zote itakua ni sehemu ya hatari kwa wanaodhani wanadamu wa JF ni tofauti na wanadamu wa kwenye mitandao mingine.
Pole Husninyo na asante kwa kushare .