Hata mimi nilikuwa sijawahi kufikiria but then again sisi wengine huwa tunaitwa wakorofi kwa hiyo uswahiba swahiba wa kwenye vi PM huwa hatuna. I guess kuna watu huwa wanaogopa kututumia PM.
Ila najua kuna watu huwa wanatumiana sana PMs. Tatizo ni kwamba watu huwa hawana siri kihivyo, Na watu wasibweteke na kudhani kuwa hizo PM ni "private" kihivyo.
Hata mimi nilikuwa sijawahi kufikiria but then again sisi wengine huwa tunaitwa wakorofi kwa hiyo uswahiba swahiba wa kwenye vi PM huwa hatuna. I guess kuna watu huwa wanaogopa kututumia PM.
Ila najua kuna watu huwa wanatumiana sana PMs. Tatizo ni kwamba watu huwa hawana siri kihivyo, Na watu wasibweteke na kudhani kuwa hizo PM ni "private" kihivyo.
hizi ni robo tu ya drama za humu lol
halafu we uliposema unanipenda sijaelewa
ndo unataka nikuharibie usichana wako au vipi?lol
Kama ulikuwa huamini, basi amini kuanzia leo kuwa behind the scene kuna mambo mengi sana yanafanyika mazuri na mabaya vikiwemo vioja vyote tuvishuhudiavyo mitaani!! Kuna watu wakianikwa humu utastaajabu nakwambia......
Najaribu kupiga hesabu, Husninyo kasema kibabu kina umri mara tatu yake..Hebu tudhani kwamba Husn ni kijana (si lazima kumuamini) ana miaka 25..kwa hiyo ni 25x3=75 (umri wa kibabu).
Lakini pia tufikiri tena, ujana unaishia 30's mwishoni....sasa let say Husn ana miaka 35 kwa hiyo inakuwa 35 (Husn) x 3 = 105.Kwa hiyo mpendwa wetu Husn alikutana na au kufanya socialisation (tafsiri kwa kiswahili) na kibabu kinachoweza kumzaa Robert Mugabe..duh!!
Lakini nimpongeze Babu maana kama ameweza kumtoa binti (kijana?) kwenye forum na kumliza si jambo dogo! Haya mengine ya mkopo ni nyongeza tu.
Unawasiliana na mtu humfahamu/hujamuona na mnaongea mambo mengi ya heri,lakini eti ghafla mnapokutana na kumuona akiwa mzee umuhimu wake unapotea?
JF ni sehemu ya kipekee ambayo kama mtu hujui hatari za mtandaoni ni rahisi kujikuta sehemu usiyoitegemea.Humu kuna wanaopiga wake zao kila siku lkn wakiwa hapa watalaani wanaume wanaopiga wake zao,kuna waliooa na wanawatoto lkn siku zote wakiwa hapa watapozi kama single men,humu kuna mashoga na wasagaji lkn wakiwa hapa watalaani hivyo vitendo,humu kuna wavivu wasipenda kujishughulisha wanaringia mali za kaka lkn wakiwa humu posts zao ni zaweza kuwa za maana kiasi ukadhani ni watu wa maana kama vitu wanavyoviandika,kuna wengine tunajifanya tumeokoka kumbe tunatype huku mkono mmoja umeshika red wine.Pia hapa JF kuna tuna utamaduni wetu fulani wa kumjua na kumpicture mtu kutokana na posts zake,kama anaonekana wa maana kutokana na vitu vya maana anavyoandika na hii inawafanya wengi tujisahau na kujikuta tunawaamini kiasi cha kuwaleta hawa watu katika maisha yetu ya kweli,mwisho wake ndo hivi vilio.JF siku zote itabaki kuwa salama kwa wenye kujua nini hatari za kwenye mitandao na siku zote itakua ni sehemu ya hatari kwa wanaodhani wanadamu wa JF ni tofauti na wanadamu wa kwenye mitandao mingine.
Pole Husninyo na asante kwa kushare .
Tangulia husn tangulia,
Bishanga Abashaija anafuata nyuma,
pembeni namwona TF anachekelea,
Anakumbuka kasheshe ya sadaka,
Bishanga sikubali,
Nami namfuata husn,
Iweje Lizzy apigwe ban?
Na bishanga aangalie tu?
Husn tusikubali,
Kweli tuondoke zetu,
TF akitaka atufuate,
Akitaka aache.
Unawasiliana na mtu humfahamu/hujamuona na mnaongea mambo mengi ya heri,lakini eti ghafla mnapokutana na kumuona akiwa mzee umuhimu wake unapotea?
How??? Nichange fone no, name n everything? It is impossible. I hope no damage will be done, kwa muda ninamuamini niliyempa!
Mkuu kwa hizo calculations inaonyesha tuna members wazee sana hapa JF.
Husny utakimbia jf kwa ID tuliokuzoea kwa ajili ya kuanza ukurasa mpya? Kwa nini
usianze ukurasa mpya kwa kuweka settings mpya hapa jf. No pm from members na hao
unao wafahamu na mna contact mnaendelea kama kawaida. Huona kama unawanufaisha hao
waliokusababisha uondoke hapa? Huko uraiani inakuaje ukichemka na kufanya mistakes,
unatafuta maisha mapya na kuhama kabisa mji na makazi? Maneno yako inaonesha umesha amua,
sisikitiki kuondoka kwako sababu wote huwa tunaondoka kwa sababu mbali mbali hasa majukumu
ila nasikitika kuondoka kwako sababu mtu kwenye key bod kakuharibia mudi ya kuwepo hapa.
Kuonesha kweli umemature ungeendelea na hio hio ID ila na taratibu na misimamo mipya
tokana na mafunzo uliopata kwenye hizo challenge zako.
Mwenzio kaolewa na kapewa sharti la kujitoa JF hivi vingine vyote ni visingizio tu! Kwa heri mway tutaonana. Tutakukumbuka kwa vimbwanga vyako.....bwah hwa hahahahahaaa
Si wazee tu..tuna waongo,wakweli na wahalifu wa mapenzi pia.Ndio maana huwa nasoma katikati ya mistari..mara nyingi unakuta story/taarifa za uongo zimewekwa humu.Au unasoma na kuamini ni story ya kweli kwa ujumla wake lakini mengine yametiwa chumvi au upotoshaji.
Hili limechangiwa sana na wasomaji kupenda ishu zisizoumiza kichwa - Story ya fasta fasta inayosisimua na majibu ya fasta fasta..ukweli utajulikana mbele ya safari.
Yote kwa yote hii ni jumuiya ya watu wengi unaweza kuiita Jumuiya ya wasiotabirika (maadam hatuonani..mwenye sura mbaya atajionyesha mzuri sana...mzuri sana lakini bogus atajionyesha ana akili nyingi....mwenye kazi ya kawaida tu atajifanya anatoka ofisi kubwaa.....Bila kusahau mzembe kitandani atajionyesha ni mahiri kwenye ngono!!!! Akili mkichwa).