Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Kiungo mchezaji , Clatous Chama, ameibua gumzo kubwa kwenye ulimwengu wa soka nchini baada ya kutishia kuweka wazi ushahidi wa mazungumzo ya faragha (chat) kati yake na Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said.
Chama anadai kuwa wakati wa mchakato wa usajili wake uliomng'oa kutoka kwa watani zao wa jadi, Simba SC, alifanyiwa shinikizo na kulazimishwa kukubali baadhi ya masharti ya mkataba huo ambayo kwa sasa yanaonekana kuleta mgongano wa kimaslahi.
"Nadhani nimetulia vya kutosha, na sasa kuna watu wanaovuka mipaka kwenye mitandao ya kijamii.
jambo moja ni hakika kuna ukweli, na kuna watu wanaozungumza ili mradi tu wasikike, labda kwa ajili ya kupata 'likes' na Comments. Lakini naamini kuwa kusimama na kusema ukweli hakupaswi kupotoshwa na kutumiwa kama dhihaka dhidi yangu, mimi ambaye nina ukweli na ushahidi wote. Ni ama tufanye hivi kwa ajili ya burudani au muache kabisa. Ninaweza kucheza mchezo huu siku nzima na bado nitasimamia ukweli kwa nini kipindi changu cha 'podcast' kiliwatia hofu,.?
Andika chapisho jingine, nami nitaweka mazungumzo yote hapa." Amesema hayo chama.