DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Mnamo jana, naibu katibu mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo Bw Benson Kigaila aliongea na vyombo vya habari ambapo aliezea mambo ambayo lazima yatekelezwe ili kama wana CHADEMA, waweze kushiriki vikao ambavyo msajili wa vyama vya siasa amepanga kufanya. Katika mambo ambayo Benson Kigaila aligusia na kusema kwamba lazima yafanyike ni pamoja na
1. Zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara liondolewe
2. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aachiliwe
3. Wana CHADEMA wengine ambao wapo mahabusu tofauti nchini waachiwe
Kwanza kabisa, nina amini kwamba haki ya kujieleza ipo kwenye katiba yetu ila jambo ambalo sielewi ni sababu ya vyombo vya usalama kuhusika kwenye kuwa kamata na kuzuia mikutano ya hadhara au mikusanyiko ya aina yoyote inayofanywa na wana CHADEMA. Vile vile bado kesi za Freeman Mbowe na wana CHADEMA wengine walio kamatwa nchini hazija sikilizwa. Kwasababu hizo sidhani kama matakwa ya wana CHADEMA yanatekelezeka haswa katika muda wanaotaka haya yote kufanyika.
Inawezekana kabisa kwa msajili wa vyama vya siasa kuwa na nia nzuri kwa kuchukua hatua hii ya kuzungumza na wahusika wote wakiwemo polisi na wana CHADEMA lakini maswali mengine ya kujiuliza ni kama kweli wana CHADEMA wanataka kufanya maridhiano, kama kweli wanafahamu kwamba matakwa yao hayatekelezeki.
Siasa safi, ambazo kila chama kina wafuasi wake na kila chama kina heshimu maamuzi ya chama kingine ni kitu ambacho kinawezekana na jitihada kama hizi za kujenga mahusiano chanya kati ya washika dau wote ni mwanzo wa hatua njema.
Kama "Chama cha Demokrasia na maendeleo", huwezi kupungukiwa chochote kwa kukaa chini kwa muda usiozidi masaa mawili au matatu kusikiliza maoni ya mtanzania mwenzako aliye upande wa pili.
Inawezekana kwamba wana CHADEMA hawaelewi kuwa maandamano yote na hasira waliyonayo vinaweza kuelekezwa kwa IGP Sirro mezani wakiwa wanaongea naye ana kwa ana na sio kwenye mitandao. Ladba ni kweli, Uanaharakati hauna tofauti sana na ushabiki wa mpira, Chama cha Demokrasia na maendeleo kinaendeshwa kwa fujo na bila mantiki.