Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaendeshwa kwa fujo na vitisho baridi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaendeshwa kwa fujo na vitisho baridi

Wengine wanadhani mambo ya siasa yanafanana na ushabiki wa mpira mitaani, tuwahurumie tu .Watanzania wanaelewa na sio wajinga kushabikia vitu wanavyoona haviana manufaa kwao ndio maana ukiwaambia waandamane huwaoni.
 
Nccr mageuzi yaliwakuta haya,Cuf waliyapata mazila haya na sasa Chadema ndio inayopata haya mazila. Inaonesha ccm wanaongopa sana chama kikuu cha upinzani ndio maana hutumia nguvu zote ili kufifisha upinzani. Katiba iliopo sasahivi ni ya ccm sisi tunataka katiba mpya tu. Mbona ccm wana ogopa kuna nini kwani hata waogope katiba mpya?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
na CDM walifanya nini kuepuka hayo?

wali relax

wabish

wajuaji
 
Turudi kwenye mstari Ukweli Watanzania wengi Wana chuki na maumivu makubwa mioyoni mwao.Tusiwe wanafiki , nchi yetu haina sababu kuwa na wafungwa wa kisiasa Ni uhuni na laana za mizimu ya wachache.
Matumizi mabaya ya dola
 
Wanabodi,

Mnamo jana, naibu katibu mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo Bw Benson Kigaila aliongea na vyombo vya habari ambapo aliezea mambo ambayo lazima yatekelezwe ili kama wana CHADEMA, waweze kushiriki vikao ambavyo msajili wa vyama vya siasa amepanga kufanya. Katika mambo ambayo Benson Kigaila aligusia na kusema kwamba lazima yafanyike ni pamoja na

1. Zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara liondolewe
2. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aachiliwe
3. Wana CHADEMA wengine ambao wapo mahabusu tofauti nchini waachiwe

Kwanza kabisa, nina amini kwamba haki ya kujieleza ipo kwenye katiba yetu ila jambo ambalo sielewi ni sababu ya vyombo vya usalama kuhusika kwenye kuwa kamata na kuzuia mikutano ya hadhara au mikusanyiko ya aina yoyote inayofanywa na wana CHADEMA. Vile vile bado kesi za Freeman Mbowe na wana CHADEMA wengine walio kamatwa nchini hazija sikilizwa. Kwasababu hizo sidhani kama matakwa ya wana CHADEMA yanatekelezeka haswa katika muda wanaotaka haya yote kufanyika.

Inawezekana kabisa kwa msajili wa vyama vya siasa kuwa na nia nzuri kwa kuchukua hatua hii ya kuzungumza na wahusika wote wakiwemo polisi na wana CHADEMA lakini maswali mengine ya kujiuliza ni kama kweli wana CHADEMA wanataka kufanya maridhiano, kama kweli wanafahamu kwamba matakwa yao hayatekelezeki. Siasa safi, ambazo kila chama kina wafuasi wake na kila chama kina heshimu maamuzi ya chama kingine ni kitu ambacho kinawezekana na jitihada kama hizi za kujenga mahusiano chanya kati ya washika dau wote ni mwanzo wa hatua njema. Kama "Chama cha Demokrasia na maendeleo", huwezi kupungukiwa chochote kwa kukaa chini kwa muda usiozidi masaa mawili au matatu kusikiliza maoni ya mtanzania mwenzako aliye upande wa pili. Inawezekana kwamba wana CHADEMA hawaelewi kuwa maandamano yote na hasira waliyonayo vinaweza kuelekezwa kwa IGP Sirro mezani wakiwa wanaongea naye ana kwa ana na sio kwenye mitandao. Ladba ni kweli, Uanaharakati hauna tofauti sana na ushabiki wa mpira, Chama cha Demokrasia na maendeleo kinaendeshwa kwa fujo na bila mantiki.
Uongo hautakusaidia lolote
 
Nimecheka kwa nguvu, eti Cdm walikuwa na hoja 2015 kushuka chini. Maoni haya ni ya wanaccm wote, utasikia huko Cdm aliyekuwa na hoja ni Dr.Slaa, lakini wakati wa Dr. Slaa ndio Cdm ilichafuliwa sana kwa ukristo, uchaga, uongo, fujo, maandamano nk. Hivyo sishangai haya maoni yako ya bendera fuata upepo.
Hahaha! Sawa Bwana Tindo, tulizoea huko nyuma likitokea jambo lolote kubwa linalogusa wananchi na serikali moja kwa moja CDM walikuwa wanaitisha press na kulizungumzia kwa undani, Juzi NKM kafanya press huku jana yake tu taifa limetangaza kupokea 1.3 trl from IMF na wakatangaza pia matumizi ya hiyo hela na mgawanyo kwa bara na visiwani, katika press yake hiyo fupi sana ilijaa tu Mbowe, Msajili na mikutano ya hadhara!! Hakugusia hilo suala la fedha hata kidogo, CDM ya zamani haikuwa hivyo, wangehoji na wangechambua hayo matumizi, wangekosoa, kushauri na kupongeza panapopongezeka!! Wenzao CCm nao wameitisha press jana, sehemu kubwa ya hiyo press wamezungumzia hilo suala la fedha!! Ni kama mmeshindwa/mmechoka kufanya kile ambacho chama kikuu cha upinzani inabidi kifanye!! Masuala kama bei ya mahindi, wamachinga, bei ya mbolea kuwa juu, vitu kupanda bei hamjawahi kuyaitia press hata siku moja!! Nyie ni Mbowe, Mbowe, Mbowe!! Kama mmeshindwa kazi kaeni pembeni, mkileta vurugu mtavunjwa viuno
 
Nani mwenye hoja kwa CDM hii ya sasa iliyojichokea? CDM walikuwa na hoja kuanzia 2015 na kushuka chini, hii ya sasa wamejaa wapotoshaji, wakurupukaji, wutukanaji, wazushi na wapinga kila kitu! May be Mkiti ila naye hana back up siku hizi, Mnyika since Lowasa alivyopokelewa kapoa sana! Hawa wengine akina Heche, Lema, Msigwa, Sugu, Pambalu, Kigaila, Lissu hamna lolote wajualo zaidi ya kupayuka majukwaani na uongo! I cant believe nimewahi kuwa die hard fan wa Lissu, Lissu viwango vimeshuka sana kwa sasa, na hivi anavyojiexpose kila siku kwenye "vispaces" uchwara vya wasaka tonge ndiyo anazidi kujishushia thamani yake na kuonesha jinsi gani mweupe kichwani! Kiongozi wa chama kikubwa lazima uwe adimu kupatikana, hata kushiriki mijadala mitandaoni lazima upunguze, sababu unachoongea pale watu wanachukulia chama ndiyo kimeongea hata kama siyo!! Mwisho wa siku anaambiwa hana adabu na "mwanaCCM" Fatma
CC😡chadema Chadema Diaspora

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Chadema madai yao mengine yanachekesha Kama hili la kutaka Mbowe aachiwe haraka, kitendo Cha Mbowe kupewa kesi ya ugaidi tayari kimemchafua hasa ukifatilia kauli ya igp. Njia pekee ya kumsafisha ni mahakama ni vema wangedai kesi isikilizwe haraka na haki kutolewa mapema badala ya kutaka aachiwe.
 
Hahaha! Sawa Bwana Tindo, tulizoea huko nyuma likitokea jambo lolote kubwa linalogusa wananchi na serikali moja kwa moja CDM walikuwa wanaitisha press na kulizungumzia kwa undani, Juzi NKM kafanya press huku jana yake tu taifa limetangaza kupokea 1.3 trl from IMF na wakatangaza pia matumizi ya hiyo hela na mgawanyo kwa bara na visiwani, katika press yake hiyo fupi sana ilijaa tu Mbowe, Msajili na mikutano ya hadhara!! Hakugusia hilo suala la fedha hata kidogo, CDM ya zamani haikuwa hivyo, wangehoji na wangechambua hayo matumizi, wangekosoa, kushauri na kupongeza panapopongezeka!! Wenzao CCm nao wameitisha press jana, sehemu kubwa ya hiyo press wamezungumzia hilo suala la fedha!! Ni kama mmeshindwa/mmechoka kufanya kile ambacho chama kikuu cha upinzani inabidi kifanye!! Masuala kama bei ya mahindi, wamachinga, bei ya mbolea kuwa juu, vitu kupanda bei hamjawahi kuyaitia press hata siku moja!! Nyie ni Mbowe, Mbowe, Mbowe!! Kama mmeshindwa kazi kaeni pembeni, mkileta vurugu mtavunjwa viuno
Chadema imeshindwa kujiendesha Kama taasisi, Mambo mengi yamesimama kisa Mbowe amekamatwa hata mkutano wa Baraza kuu wameusimamisha hili ni tatizo kubwa swala la tozo walikaa kimya.
 
Chadema imeshindwa kujiendesha Kama taasisi, Mambo mengi yamesimama kisa Mbowe amekamatwa hata mkutano wa Baraza kuu wameusimamisha hili ni tatizo kubwa swala la tozo walikaa kimya.
Wapo kimya, kwa sasa hatujashuhudia press yeyote imezuiwa, watumie njia hiyo na waite vyombo vya habari makini, wao wanafanya press utafikiri press ya Majimaji ya Songea, vimike vitatu vya youtube channels chovuchovu, mwongeaji anaongea dkk 15, atongelea Mbowe, Sirro, Msajili, Mikutano ya hadhara, anajibu swali moja la DarMpya TV, Press imeisha!! Ukiwaambia wanakuita MATAGA, wengine watakuambia una mimba, wengine watakuita mpuuzi na mpumbavu
 
Hivi msajili wa vyama vya siasa kazi zake ni zipi?
Polisi kazi yake ni kuzuia mikutano na maandamano au kulinda usalama wa watu na mali zao?, Je kwanini mikutano na maandamano yanayozuiliwa ni ya vyama vya upinzani tu na sio CCM?
Je vyama vya siasa kazi zake ni zipi, je sheria zinasemaje kuhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na maandamano au makongamano?
 
Nccr mageuzi yaliwakuta haya,Cuf waliyapata mazila haya na sasa Chadema ndio inayopata haya mazila. Inaonesha ccm wanaongopa sana chama kikuu cha upinzani ndio maana hutumia nguvu zote ili kufifisha upinzani. Katiba iliopo sasahivi ni ya ccm sisi tunataka katiba mpya tu. Mbona ccm wana ogopa kuna nini kwani hata waogope katiba mpya?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Hawaogopi katiba mpya kwa sabab wao ndio waandish na wataiandika kwa namna wao wanataka na kuna uwezekano mkubwa isitofautiane saaaaana na hii ya sasa na ndio maana wanaipotezea
 
Hao wakulima wao ni mabubu hawawezi kulalamikia bei ya mbolea na kukosa bei nzuri kwa mazao yao?
! SaHwa Bwana Tindo, tulizoea huko nyuma likitokea jambo lolote kubwa linalogusa wananchi na serikali moja kwa moja CDM walikuwa wanaitisha press na kulizungumzia kwa undani, Juzi NKM kafanya press huku jana yake tu taifa limetangaza kupokea 1.3 trl from IMF na wakatangaza pia matumizi ya hiyo hela na mgawanyo kwa bara na visiwani, katika press yake hiyo fupi sana ilijaa tu Mbowe, Msajili na mikutano ya hadhara!! Hakugusia hilo suala la fedha hata kidogo, CDM ya zamani haikuwa hivyo, wangehoji na wangechambua hayo matumizi, wangekosoa, kushauri na kupongeza panapopongezeka!! Wenzao CCm nao wameitisha press jana, sehemu kubwa ya hiyo press wamezungumzia hilo suala la fedha!! Ni kama mmeshindwa/mmechoka kufanya kile ambacho chama kikuu cha upinzani inabidi kifanye!! Masuala kama bei ya mahindi, wamachinga, bei ya mbolea kuwa juu, vitu kupanda bei hamjawahi kuyaitia press hata siku moja!! Nyie ni Mbowe, Mbowe, Mbowe!! Kama mmeshindwa kazi kaeni pembeni, mkileta vurugu mtavunjwa viuno
 
Hahaha! Sawa Bwana Tindo, tulizoea huko nyuma likitokea jambo lolote kubwa linalogusa wananchi na serikali moja kwa moja CDM walikuwa wanaitisha press na kulizungumzia kwa undani, Juzi NKM kafanya press huku jana yake tu taifa limetangaza kupokea 1.3 trl from IMF na wakatangaza pia matumizi ya hiyo hela na mgawanyo kwa bara na visiwani, katika press yake hiyo fupi sana ilijaa tu Mbowe, Msajili na mikutano ya hadhara!! Hakugusia hilo suala la fedha hata kidogo, CDM ya zamani haikuwa hivyo, wangehoji na wangechambua hayo matumizi, wangekosoa, kushauri na kupongeza panapopongezeka!! Wenzao CCm nao wameitisha press jana, sehemu kubwa ya hiyo press wamezungumzia hilo suala la fedha!! Ni kama mmeshindwa/mmechoka kufanya kile ambacho chama kikuu cha upinzani inabidi kifanye!! Masuala kama bei ya mahindi, wamachinga, bei ya mbolea kuwa juu, vitu kupanda bei hamjawahi kuyaitia press hata siku moja!! Nyie ni Mbowe, Mbowe, Mbowe!! Kama mmeshindwa kazi kaeni pembeni, mkileta vurugu mtavunjwa viuno
Chadema wameamua kupambana kivyao, hawataki kupambania wananchi.
 
Umeandika dude refu lisilo na akili,
Umejiuliza yafuatayo?
1.polisi wanahusika kwenye siasa?
2. Polisi kwanini hawaheshimu katiba badala yake wanaiheshimu ccm tu?
3. Kuwaachia wana chadema waliowabambikia kesi kunahitaji maridhiano gani?

Panasiku polisi na ccm watalipa kwa haya wanayoyafanya kwa wananchi wanaowanyanyasa eti kisha waendelee kubaki madarakani

HAKUNA JAMBO LISILO NA MWISHO

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Nina kubaliana na wewe unaposema kwamba maamuzi yanayofanywa na polisi hayaendani na yaliyomo kwenye katiba. Sambamba na hayo nina amini sana katika mikakati inayo anzishwa kutatua changamoto zilizopo. Sidhani kama wana CHADEMA walifanya maamuzi sahihi kwa kuamua kususia mikutano iliyopangwa na msajili wa vyama vya siasa na inawezekana kabisa kwamba walifanya hivyo ili kuhakikisha kwamba vugu vugu lililopo lisipoe. Kuishi vizuri na serikali, bila fujo za hapa na pale ni kitu ambacho hakiwa saidii sana wana CHADEMA
 
Unaweka Post bila kujua tatizo liko wapi, angalau ungejua hata sheria na kanuni zinazoruhusu vyama vya siasa kufanya siasa nchini, hata hilo haulijui ila unajua kulaumu usilolijua! Fanya utafiti kabla ya kuweka Post ili watu wajadili hoja zako.
Ndugu,
Swala la msingi hapo liko wazi kuwa uongozi wa NCHI hii umeshindwa na wanauogopa utawala bora.
Mpaka sasa anaevunja katiba hii iliyopo na hata sheria mbovu zilizopo, anajulikana ni Polisi. Ambao wameamua kujiingiza kwenye siasa
Sasa hayo mazungumzo nae ya nini? Kujadiliana nae kitu gani cha msingi?
Katiba mpya ndio yatakiwa kuwa DAWA ya ubabaishaji huu.
 
Wengine wanadhani mambo ya siasa yanafanana na ushabiki wa mpira mitaani, tuwahurumie tu .Watanzania wanaelewa na sio wajinga kushabikia vitu wanavyoona haviana manufaa kwao ndio maana ukiwaambia waandamane huwaoni.
Pole ndugu,
Katiba mpya ndio dawa hasa kwenu mnaoimbishwa nyimbo za watoto wa chekechea
 
Back
Top Bottom