Chama cha Madaktari Tanzania watoa Tamko Juu ya Kukamatwa kwa Dkt. Conrad Agonza Kahyoza

Chama cha Madaktari Tanzania watoa Tamko Juu ya Kukamatwa kwa Dkt. Conrad Agonza Kahyoza

Serikali itaamua kimya kimya kuhusu watumsihi wake, wote wanae. Tena mmoja ni Bingwa, haitakubali impoteze.
 
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kinondoni, namba F. 8886 SGT Andrew, ameshambuliwa kwa ngumi na mateke na dereva Conrad Agonza Kayoza (35), Daktari Bingwa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na mkazi wa Lugalo na Mloganzila, wakati akitekeleza majukumu yake ya kisheria.

Tukio hilo limetokea jana, Septemba 8, 2026, majira ya saa 1:30 asubuhi katika eneo la Lugalo, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam.

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema kimepokea taarifa kuhusu tukio lililotokea Jana tarehe 8 Septemba 2026 katika eneo la Lugalo, Kinondoni, Dar es Salaam, linalomhusisha Dkt. Conrad Agonza Kahyoza ambaye ni Daktari Bingwa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na Askari wa Usalama Barabarani mwenye namba F.8886 SGT.

Baada ya tukio hilo, uongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) umefanya mazungumzo na Jeshi la Polisi Tanzania kupitia, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Murilo, na kufahamishwa kwamba Dkt. Agonza alipata majeraha na kupelekwa haraka hospitalini kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya dharura na hali yake imeimarika. Kwasasa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay na taratibu za kisheria zinaendelea.

MAT imesma kwa kuzingatia hali ya Dkt. Agonza na mahitaji yake ya matibabu, MAT inaendelea kufuatilia kwa karibu ustawi wake na kuhakikisha kwamba anapata huduma stahiki za matibabu kwa wakati wowote atakapohitaji.

Aidha Uongozi wa MAT kupitia wanasheria wake unaendelea kufuatilia taratibu za kisheria kuhakikisha anapata msaada wa kisheria wa haraka ikiwa ni pamoja na dhamana.
SaveClip.App_801304789_18007574600970473_736828196592309066_n.webp
 
Bwana mganga bingwa anasema shida nini....?
 
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimepokea taarifa kuhusu tukio lililotokea tarehe 8 September 2026 katika eneo la Lugalako, Kinondoni, Dar es Salaam, linalomhusisha Dkt. Conrad Agonza Kahyoza ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila na Askari wa Ulinzi wa Barabarani mwenye namba F.8886 SGT.

Baada ya tukio hilo, uongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) umefanya mazungumzo na Jeshi la Polisi Tanzania, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muro, na kufahamishwa kwamba Dkt. Agonza alipata majeraha na kupelekwa haraka hospitalini kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya dharura na hali yake imeimarika. Kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay na taratibu za kisheria zinaendelea.

Chama cha Madaktari Tanzania kinamsisitizia yafuatayo:

Kwanza:
kwa kuzingatia hali ya Dkt. Agonza na mahitaji yake ya matibabu, MAT inaendelea kufuatilia kwa karibu ustawi wake na kuhakikisha kwamba anapata huduma stahiki za matibabu kwa wakati wote atakapohitaji.

Pili: Uongozi wa MAT kupitia wanasheria wake unaendelea kufuatilia taratibu za kisheria kuhakikisha anapata msaada wa kisheria wa haraka ikiwa ni pamoja na dhamana.

Tatu: MAT kwa kushirikiana na muajiri wa Dkt. Agonza (Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila) pamoja na familia itaendelea kufuatilia na kutoa taarifa kulingana na mwenendo wa shauri hili.

Soma Pia: Polisi: Conrad Agonza Kayoza anashikiliwa kwa kumshambulia kwa ngumi na mateke Askari wa Usalama barabarani

Chama cha Madaktari Tanzania kinaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu na kitaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa mamlaka husika, huku kikilinda maslahi, utu na haki za mwanachama wake kwa mujibu wa sheria.

View attachment 3666217
Polisi wasituchanganye hapa ,ilikuwaje dakatari akapata majera wakati wao wanamshitaki kwa kumpiga polisi,inammana na yeye alijipiga mwenyewe
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
KAMA AMBULANCE INARUHUSIWA KUPITA SERVICE ROAD HALAFU GARI YA DAKTARI INAZUIWA DOES IT MAKE SENSE?
KAMA GARI ZA WANASIASA ZINARUHUSIWA HOW COMES YA DAKTARI ISIRUHUSIWE,KATI YA MWANASIASA NA DAKTARI NI YUPI ANAWAHI DHARURA YA KWELI?
 

Attachments

  • AMBULANCE.jpg
    AMBULANCE.jpg
    56.8 KB · Views: 9
SIO rahisi KWA daktari kumpigana kwa maadili ya kazi yake na kiapo chake,hakuna daktari anahepiga watu ila anatibu watu,na inawezekana alitukanwa matusi mabaya ama alipokonywa funguo ya gari huku akitukanwa matusi,hivyo katika kuchukua funguo ya gari yake Kali yake ili awahi kwenda kutimiza majukumu yake ndipo sasa Waka angushana katika kupokonyana funguo ya gari,HAKUNAGA DAKTARI ANAYEPIGA WATU,hapo daktari alicheleweshwa kwenda kutimiza majukumu yake ya kuhudumia wagonjwa.DAKTARI YEYOTE HAWEZI KUPIGA WAGONJWA WAKE.
 
Back
Top Bottom